Quran
-
Je, Qur’ani Imeruhusu Kuoa Zaidi ya Mke Mmoja?
Swali muhimu hapa ni hili: Je, mwanadamu anaweza kutekeleza uadilifu kamili miongoni mwa wake wengi? Jibu linatolewa na Qur’ani yenyewe katika Aya ya 129 ya Suratu An-Nisaa: «وَلَنْ تَسْتَطِیعُوا أَنْ تَعْدِلُوا بَیْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ» (Kamwe hamtaweza kuwa na uadilifu kamili miongoni mwa wanawake, hata mkijitahidi kwa dhati). Kwa hiyo, kwa mtazamo wa Qur’ani, uadilifu kamili miongoni mwa wake ni jambo lisilowezekana, au angalau ni jambo gumu sana kutekelezeka. Wakati Mwenyezi Mungu Mwenyewe anaposema kwamba kutimiza sharti hili haiwezekani, basi “hofu ya kutotenda kwa uadilifu” si uwezekano wa mbali, bali ni hali inayoweza kuwepo daima. Kwa hiyo, hukumu ya mwisho, yaani «أَدْنَیٰ أَلَّا تَعُولُوا» (ili iwe karibu zaidi na kutofanya dhuluma), itakuwa kuwa na mke mmoja.
-
“Diplomasia ya Aya”: Aya za Qur'ani zilizosomwa katika marasimu ya mazishi ya Kiongozi Shahidi Imam Sayyid Ali Khamenei zavutia hisia za wengi
Katika marasimu ya kuuaga mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Sayyid Ali Khamenei (Quds Sirruh), uteuzi wa Aya za Qur'ani Tukufu zilizosomwa kwa kila ujumbe wa wageni waliotoa salamu za rambirambi ulivutia hisia za wengi, huku kila Aya ikionekana kubeba ujumbe maalumu wa kisiasa, kiitikadi na kiroho.
-
Mfululizo wa Mwitikio dhidi ya Kudharau Qur’ani Tukufu; Hizbullah:Marekani na Lobi ya Kizayuni Ndio Wahusika Wakuu wa Kuitukana Mitakatifu ya Waislamu
Hizbullah ya Lebanon katika tamko lake imesisitiza kuwa: “Utamaduni wa ubaguzi wa rangi na hotuba za chuki, ambazo zimekuwa zikichochewa na mikondo ya kisiasa na vyombo vya habari vya Magharibi kwa msukumo wa tawala mfululizo za Marekani na lobi za Kizayuni kwa miongo kadhaa, zimefanya juhudi za makusudi za kupotosha taswira ya Uislamu. Hatua hizi zinafanywa kwa ajili ya kutumikia miradi ya fitna, ukoloni na uharibifu, na ndizo sababu kuu zilizowapa ujasiri watu wenye misimamo mikali kufanya vitendo hivi vya aibu.”
-
Shukrani za Ayatollah Nouri Hamadani kwa jitihada za Ofisi ya Vikundi vya Misikiti katika shughuli za Qur’an / Ihitaji uwepo mkubwa zaidi wa vijana katika Misikiti.
Kiongozi wa kiitikadi wa Mashia alisema kuwa: ‘Msikiti usio na vijana hauwezi kustawi, na uwepo wa vijana katika misikiti ni wa thamani sana.’ Alisisitiza: ‘Ninashukuru na kupongeza jitihada za Vikundi vya Utamaduni na Sanaa vya Misikiti katika shughuli za Qur’an na uhai wa misikiti, na nina matumaini uwepo wa vijana katika misikiti utakuwa mkubwa zaidi.