Kuongezeka kwa uwepo wa kijeshi wa Misri katika Sinai na ushirikiano wa kimkakati na China, kumeanzisha mgogoro mpya kati ya Cairo na Tel Aviv na kuweka hatarini mustakabali wa mkataba wa amani wa Camp David.
Shirika la Redio na Televisheni la utawala wa Kizayuni limedai kwamba Misri, sambamba na kuongezeka kwa operesheni za kijeshi za Israel huko Gaza, imetuma maelfu ya wanajeshi na vifaa vya kijeshi katika eneo la kaskazini mwa Jangwa la Sinai lililoko mpakani na Ukanda wa Gaza na Israel.