Tamaa
-
Ayatullah Javadi Amoli alisema:
“Iwapo kitovu cha mgawanyiko kitaundwa kati ya taifa na serikali, msingi wa mfumo utadhurika”
Mmoja wa maraji wa juu wa Washia alisema: “Iwapo kitovu cha mgawanyiko kitaibuka kati ya serikali na taifa, msingi wa mfumo utadhurika. Iwapo kiongozi atakuwa na wavurugiko kati ya matakwa yake ya kimaakili na tamaa za nafsi, ataondoka mbali na haki.”
-
Maneno Mafupi, Yenye Maana Pana:
Hotuba ya 21 ya Nahjul Balagha: "Kuwa na mzigo mwepesi ili mfike (kwenye safari yenu)!"
تَخَفَّفُوا تَلْحَقُوا، فَإِنَّمَا يُنْتَظَرُ بِأَوَّلِكُمْ آخِرُكُمْ "Punguzeni mizigo ili mfike (kwenye malengo ya safari yenu), kwa maana waliotangulia wanawasubiri mlio nyuma." Hotuba ya 21 ya Nahjul Balagha – Mtazamo wa Akhera katika Jitihada za Binadamu: Hotuba ya 21 ya Nahjul Balagha inaangazia maisha ya binadamu kwa mtazamo wa akhera, na inaeleza kwamba: Binadamu anapaswa kuwa mwepesi wa mizigo (wa kidunia), ili aweze kwa urahisi kutoka duniani na kuelekea kwenye maisha ya akhera. Hili linaonyesha kuwa jitihada za binadamu si kwa ajili ya dunia pekee, bali kwa ajili ya ukamilifu wa kiutu (kamilifu) na maisha ya milele.
-
Je, Mazungumzo Kati ya Mwanamume na Mwanamke Wasiokuwa Mahramu Yamekatazwa kwa namna yoyote ile katika Uislamu?
“Kauli yenye nguvu zaidi ni hii kwamba kusikia (kusikiliza) sauti ya Mwanamke asiyekuwa Mahram, maadamu si kwa ajili ya tamaa, starehe au maslahi, ni jambo linaloruhusiwa (linajuzu). Vivyo hivyo kwa Mwanamke, ikiwa hakuna hofu ya fitina, anaweza kusikika na Wanaume wasio mahram kwake".