“Arubaini ya mwaka huu inapaswa kuleta tumaini kwa Waislamu na kuwavunja nguvu maadui. Umoja ndiyo njia ya wokovu kwa Ulimwengu wa Kiislamu na Bendera ya Mapambano dhidi ya mfumo wa kishetani lazima ibaki juu.”
Sheikh Abdul Rahman Kachere: "Mtu anayemfahamu Imam Hussein (AS) daima ni jasiri katika kukabiliana na dhulma".Kumjua vizuri Imam Hussein (as) kutawafanya watu wa mataifa mbalimbali kumpinga adui na dhalimu, na kutambua njama za adui na dhalimu dhidi ya mataifa yao, na kuwa tayari kupambana kwa ajili ya kuinusuru Haki, kwa ajili ya kuondoa uistikbari, dhulma na unyonyaji wa mfumo mpya wa ukoloni unaoitwa: Ukoloni mambo leo.