Ripoti ya Fox News imeeleza kuwa pendekezo la kuanzisha mfuko wa uwekezaji wa dola bilioni 300 kwa ajili ya ujenzi upya wa Iran linaonekana kukabiliwa na vikwazo vikubwa vya kisheria chini ya sheria za vikwazo za Marekani, na linaweza kuwa lisilotekelezeka kivitendo.
Kwa upande wake, Balozi Lentz alieleza kuwa ushirikiano wa Tanzania na Marekani umejengwa katika misingi ya ustawi wa pamoja, si utegemezi wa misaada, na kupongeza juhudi za Tanzania chini ya falsafa ya 4R na Dira ya Maendeleo ya 2050. Takribani makampuni 400 ya Marekani yanafanya kazi nchini, jambo linaloonesha kuimarika kwa mazingira ya uwekezaji.