Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi, amempokea Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan, Mohsin Naqvi, ambapo viongozi hao walijadili maendeleo ya ushirikiano wa pande mbili na utekelezaji wa makubaliano kati ya Tehran na Islamabad.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Oman wamejadili kwa njia ya simu umuhimu wa kulinda usalama wa Mlango wa Hormuz, kuimarisha usalama wa usafiri wa baharini, na kupanua ushirikiano wa pande mbili kufuatia makubaliano ya hivi karibuni kati ya Tehran na Washington.
Mkutano wa kielimu wa “Sira ya Alawi” umefanyika Chittagong, Bangladesh, kwa ushirikiano wa wanazuoni wa Shia na Sunni, ukijadili maadili, haki na uongozi wa kidini wa Imam Ali (a.s) na kuhimiza mshikamano wa kidini na kitamaduni katika jamii ya Kiislamu.