ahadi
-
Pakistan na Mtihani wa Ahadi ya Ulinzi kwa Saudi Arabia: Je, Islamabad Itatuma Vikosi Yemen?
Ushirikiano wa ulinzi kati ya Pakistan na Saudi Arabia umeingia katika hatua mpya kufuatia mkutano wa dharura wa muungano wa Makkah uliofanyika Riyadh.
-
Uturuki Yaachukua Hatua Kuanza Kutoa Msaada wa Kijeshi na Kitaalamu kwa Saudi Arabia
Uturuki imeanza kutoa msaada wa kiulinzi na kitaalamu kwa Saudi Arabia, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake chini ya Makubaliano ya Makka.
-
Serikali ya Shahidi Raisi: Urithi wa Shahidi Nasrallah Utaendelea Kuishi Hadi Kukombolewa kwa Quds
Katika kuelekea kumbukumbu ya pili ya kuondoka duniani kwa kinara wa Muqawama wa Kiislamu, viongozi wa Serikali ya Awamu ya 13 wametoa tamko wakisisitiza kufanya upya ahadi yao kwa misingi na malengo ya mashahidi wa Muqawama, pamoja na kusisitiza kuendelea kwa sera ya mambo ya nje ya kuunga mkono Muqawama, chini ya uongozi wa Kiongozi mpya na mwenye hekima wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Ayatullah A’rafi: Vyuo vya Dini vya Wanawake Vinapaswa Kushiriki katika Nyanja Zote za Sayansi za Kiislamu
Mkuu wa Vyuo vya Dini nchini amesisitiza kwamba Vyuo vya Dini vya Wanawake vina majukumu mawili, ya jumla na maalumu, na kusema: Vyuo vya Dini vya Wanawake vina nafasi katika uzalishaji, uchakataji, uendelezaji na usambazaji wa elimu katika nyanja zote za sayansi za Kiislamu, ikiwa ni pamoja na elimu ya Tauhidi, itikadi, Hadithi, Tafsiri, Fiqhi, maadili na maarifa ya Kiislamu. Aidha, sambamba na hayo, vinapaswa kuwa vinara wa kipekee katika masuala yanayohusu wanawake na familia.
-
“Tuko pamoja nawe katika ahadi hadi alfajiri ya kudhihiri”: Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku 40 ya “Shahidi wa Iran”
Kauli mbiu “Tuko pamoja nawe katika ahadi hadi alfajiri ya kudhihiri” imechaguliwa kwa ajili ya maadhimisho ya siku 40 tangu mazishi ya kiongozi aliyefariki shahidi, Ayatullah al-Uzma Sayyid Ali Husayni Khamenei. Sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika Tehran, Qom, Mashhad na miji mingine nchini Iran, sambamba na kumbukumbu ya shahada ya Imam Hasan al-Askari (as) na kuanza kwa Uimamu wa Imam Mahdi (aj).
-
Mkuu wa Mamlaka ya Mahakama Iran: Kuunga Mkono Marekani Kutawaletea Baadhi ya Watawala wa Eneo Hasara na Kushindwa
Mkuu wa Mamlaka ya Mahakama ya Iran, Hojjatul-Islam Gholam-Hossein Mohseni Ejei, amewatahadharisha watawala wanaoitegemea Marekani na kuamini ahadi za “Shetani Mkuu”, akisema kuwa hawatapata chochote isipokuwa hasara na kushindwa.
-
Ayatollah Khatami: Trump na Netanyahu Hawatakuwa na Usingizi wa Amani
Mwanachama wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Elimu ya Kiislamu ya Qom amesema kuwa ibada za mazishi ya Kiongozi aliyefariki akiwa shahidi katika maeneo mbalimbali ya nchi zimegeuka kuwa jukwaa la umoja, mshikamano na kuhuisha ahadi ya utii kwa Mapinduzi ya Kiislamu. Amesisitiza kwamba: “Trump na Netanyahu hawatakuwa na usingizi wa amani.”
-
Iran: Ukiukaji wa Ahadi za Marekani Utakabiliwa na Hatua za Kujibu
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baqaei, amesema Iran haijaomba mazungumzo na Marekani, akisisitiza kuwa sera ya Jamhuri ya Kiislamu inategemea kanuni ya "ahadi kwa ahadi" na kwamba ukiukaji wowote wa ahadi za Washington utakabiliwa na jibu la Iran.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Makubaliano kati ya Iran na Marekani Yanategemea Kanuni ya “Ahadi kwa Ahadi”
Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa makubaliano ya maelewano kati ya Iran na Marekani hayajajengwa juu ya msingi wa kuamini serikali ya Marekani, bali yanazingatia kanuni ya “utekelezaji wa ahadi kwa pande zote,” huku akisisitiza kuwa Iran haitaruhusu Marekani kuingilia masuala ya Mlango wa Hormuz.
-
Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi: Marekani Inaelewa Zaidi Lugha ya Uchumi Kuliko Ahadi za Kisiasa
Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Mohammad Mokhber, amesema Iran haitakubali makubaliano yasiyotekelezwa kikamilifu na kusisitiza kuwa haki za wananchi wa Iran pamoja na damu za mashahidi haziwezi kusahaulika.
-
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Adui Aliishambulia Iran Akidhani Atashinda, Lakini Ameambulia Kushindwa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baqaei, amesema kuwa mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya Iran kwa uungaji mkono wa Marekani yalishindwa kufikia malengo yake kutokana na uimara, mshikamano na kujitolea kwa wananchi wa Iran, hali iliyowageuzia washambuliaji hasara na kushindwa.
-
Ghalibaf: Hatuamini Ahadi za Adui, Kipimo ni Matokeo ya Vitendo
Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, amesema kuwa Iran haitategemea ahadi za maadui katika medani ya diplomasia, akisisitiza kuwa mafanikio hupimwa kwa matokeo halisi na kwamba umoja wa wananchi umechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha nafasi ya taifa hilo katika kukabiliana na mashinikizo ya nje.
-
Vyombo vya Habari vya Kiarabu Vyapongeza Ushiriki Mkubwa wa Watu katika Maandamano ya 22 Bahman ya Kumbukumbu ya Miaka 47 ya Mapinduzi ya Iran
Maandamano ya 22 Bahman kwa maadhimisho ya miaka 47 ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yameripotiwa kwa upana na vyombo vya habari vya Kiarabu. Mitandao kama Al-Mayadeen, Al-Manar na Al-Masirah pamoja na magazeti ya Ra’i Al-Youm na Al-Arabi Al-Jadeed yaliripoti ushiriki mkubwa wa wananchi katika Tehran na zaidi ya miji 1200, yakitaja hotuba ya rais kuhusu kuimarisha uhusiano na majirani na kuoneshwa kwa mafanikio ya kijeshi kama alama ya upya wa ahadi kwa malengo ya Mapinduzi.