ashura
-
Operesheni ya Kisaikolojia huko Karbala: Uchambuzi wa Kihabari wa Ujumbe wa Imam Hussein (a.s) kabla na baada ya Ashura
Mapinduzi ya Imam Hussein (a.s) hayakuwa vita vya kijeshi pekee; bali yalikuwa vita kamili vya kihabari na kisaikolojia vilivyolenga nyoyo na akili za watu. Kuanzia mahubiri ya Makka hadi ujumbe ulioandikwa kwa damu huko Karbala, Imam Hussein (a.s) aliwezaje kuhamasisha maoni ya umma dhidi ya utawala wa Yazid? Uchambuzi wa mkakati wa mawasiliano wa Imam (a.s) katika mojawapo ya nyakati nyeti zaidi katika historia ya Kishia, unaonesha mfano wa kipekee wa uanaharakati wa kihabari unaosimama juu ya ukweli.
-
Kiongozi wa Shirika la Awqaf la Iran: Arubaini ya Mwaka Huu Itakuwa na Sura ya Kupinga Uzayuni - Iran ni A'shura ya Dunia ya Leo
Arubaini ya mwaka huu si tu tukio la ibada bali ni ujumbe wa mapambano ya kimaanawi na kisiasa. Iran inachukua nafasi ya kiashura ya dunia, ambapo uongozi, mshikamano, na upinzani dhidi ya dhulma vinaonyeshwa kwa njia halisi.
-
A'shura ni ishara ya uvumilivu katika vyombo vya habari vya Bahrain, lakini kwa kweli, ni eneo la ukandamizaji dhidi ya Mashia
Mwanaharakati wa haki za binadamu wa Bahrain amesema: A'"shura inatolewa kila mwaka katika vyombo vya habari vya Bahrain kama ishara ya uhuru na uvumilivu wa kidini, lakini kivitendo wafuasi wa Kishia wanakabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria na vikwazo vikali, kuanzia kukamatwa na kuandikiwa wito hadi kuharibiwa maeneo ya kidini na mashinikizo ya kubadili mavazi ya kidini.
-
Jumuiya ya Waislamu wa Shia Khoja Ithna Ashari Jamiat katika Matembezi ya A'shura
ASHURA ni siku ya kumi ya mwezi mtukufu wa Muharram. Katika siku hii ya Ashura mjukuu wa Mtume yaani Imam Hussain (as) aliuawa katika tambarare za mji wa Karbala baada ya kusimama kidete dhidi ya mtawala dhalimu wa wakati ule, Yazid bin Muawiya, akatoa fundisho la kukataa kumpigia magoti mdhalimu huyo, ndipo akajitolea maisha yake, akauawa ili kunusuru ubinaadamu , utu pamoja na kupigania uislamu.
-
Siku ya 11 baada ya A'shura | Karbala imetenganisha Kati ya Dini ya Kuabudu Matwaghuti (Bani Umaiyya) na Dini ya Kumuabudu Mwenyezi Mungu
Dini ya Kumuabudu Mwenyezi Mungu (swt) baada ya vita vya Karbala iliwakilishwa na damu ya Imam Hussein (a.s) na Mashahidi wa Karbaka ambayo ilikuwa kielelezo hai cha dini ya haki ya Mwenyezi Mungu.