Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika kikao cha mashauriano na kamati na Mawakibu za Arubaini kilichofanyika katika miji ya Samarra na Balad nchini Iraq, Hujjatul Islam wal-Muslimin Sayyid Mahdi Khamoushi, Mkuu wa Shirika la Awqaf na Mambo ya Kheri la Iran, alisisitiza nafasi ya kiutamaduni na kiroho ya Arubaini, akiitaja kuwa ni tukio la kipekee katika dunia ya sasa.
Maelezo Muhimu kutoka kwa Hujjatul Islam Khamoushi ni kama ifuatavyo:
Arubaini ina maana nyingi kwa Waislamu, na tunapaswa kuikaribia kwa undani zaidi na kuelewa maana yake ya kweli kwa moyo wa ndani.
Idadi kubwa ya Mazuwwari wanaotembea kwa miguu kuelekea Karbala ni tukio lisilo na mfano katika historia ya sasa ya Binadamu. Imamu Hussein (a.s) ameweka njia, na sisi tunapaswa kuitikia kwa uwezo wetu wote.
Usalama wa njia za ziara ya Arubaini nchini Iraq umetokana kwa kiasi kikubwa na juhudi za vikosi vya Hashd al-Sha’abi.
Pia alisisitiza kuwa ushirikiano na wananchi wa Iraq unapaswa kuleta manufaa ya kiuchumi kwao, ili kuimarisha uhusiano wa watu kwa watu.
Alitoa wito wa mshikamano wa Kiislamu kwa kusema: “Tunawapa ndugu zetu wa Kisunni mkono wa udugu, kwa kuwa adui yetu ni mmoja.”
Alisisitiza umuhimu wa kuendeleza hija za maeneo kama Samarra na Balad, akisema kuwa mawakibu zinazofanya kazi huko ziko katika jihadi halisi, na ni juu yetu kuziongezea nguvu.
Arubaini ya Mwaka Huu: Itakuwa na Sura ya Kupinga Uzayuni na Umoja wa Kiislamu
Katika muktadha wa kisiasa na kimataifa wa mwaka huu, Hujjatul Islam Khamoushi alieleza kuwa Arubaini ya 2025 lazima iwe na sura ya wazi ya kupinga uzayuni na Marekani.
Alihimiza kwamba:
Somo la kujitolea, ushahidi, Umoja wa Umma wa Kiislamu, na uongozi wa hekima wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi linapaswa kuelezwa kwa njia sahihi.
Ni wajibu wetu kuonyesha jinsi Waislamu, kwa mshikamano wao, wameweza kuwashinda maadui wao, hususan utawala wa Kizayuni (Israel).
Alisisitiza: Arubaini ya mwaka huu si tu tukio la ibada bali ni ujumbe wa mapambano ya kimaanawi na kisiasa. Iran inachukua nafasi ya kiashura ya dunia, ambapo uongozi, mshikamano, na upinzani dhidi ya dhulma vinaonyeshwa kwa njia halisi.
Katika hali ya sasa ya Mashariki ya Kati, Arubaini ni jukwaa la kuonyesha umoja wa Umma wa Kiislamu dhidi ya uzayuni na ukoloni wa kisasa.
Your Comment