"Unaweza kumdhulumu mtu na ukalala usingizi mzito, lakini yule uliyemdhulumu halali kamwe. Anakumbuka dhulma yako kila siku na humlalamikia Mwenyezi Mungu dhidi yako. Na ikumbukwe kuwa macho ya Mwenyezi Mungu hayalali,” amesema Sheikh Ahmad Haji, akisisitiza hatari ya dua ya aliyedhulumiwa.
Rabi David Feldman aliuelekeza ujumbe wa moja kwa moja kwa vijana wa Kiyahudi wanaoishi chini ya uvamizi wa Israel, akiwataka wakimbie katika dola hilo, akionya kuwa kuendelea kwa vita vya mauaji ya kimbari hakuwahatarishi Wapalestina na Waislamu pekee, bali pia kunaongeza hatari ya chuki na vurugu dhidi ya Wayahudi katika nchi mbalimbali duniani. Pia alieleza msimamo wake kuhusu mjadala wa sasa wa suluhisho la mataifa mawili.