Tathmini nyingi kutoka ndani ya vyombo vya usalama vya Marekani zinaonyesha kuwa Iran bado ina uwezo wa kuendeleza mpango wake wa nyuklia. Badala ya kuuzuia, mashambulizi ya Marekani huenda yameifanya Iran kuwa na msimamo mkali zaidi na kufikiria kuujenga kwa matumizi ya kijeshi.
"centrifuges" (au kwa kiswahili: Visukuma ambavyo hutumika katika teknolojia ya nyuklia) zote ziko salama, na ambazo hutumiwa kimsingi kwa urutubishaji wa uranium, mchakato ambao hutenganisha isotopu za uranium ili kuongeza mkusanyiko wa U-235, ambayo huhitajika kwa vinu vya nyuklia.