Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa makubaliano ya maelewano kati ya Iran na Marekani hayajajengwa juu ya msingi wa kuamini serikali ya Marekani, bali yanazingatia kanuni ya “utekelezaji wa ahadi kwa pande zote,” huku akisisitiza kuwa Iran haitaruhusu Marekani kuingilia masuala ya Mlango wa Hormuz.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Ulinzi, Brigedia Talaeinik alibainisha kuwa Marekani na washirika wake wanasisitiza mazungumzo kuhusu programu ya makombora na wanataka kupunguza umbali wa makombora ya Iran. Hata hivyo, alisema kuwa msingi wa uwezo wa makombora ya Iran ni kulinda usalama na maslahi ya kitaifa ya wananchi wake.