Sheikh Swaleh Maulid, Khatibu wa Swala ya Ijumaa katika Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni – Tanzania, ametoa mawaidha kuhusu umuhimu wa kujenga tabia njema na kuchukua hatua za kiroho zinazomsaidia mwanadamu kujiepusha na vishawishi vya Shetani.
Vyombo vya habari vya Magharibi na Israel vimeripoti kuwa mpango wa Saudi Arabia wa kuunda muungano wa kijeshi wa baharini katika Bahari Nyekundu umekumbana na vikwazo vikubwa, huku ukitajwa kuwa hauna uwezo wa kubadili hali ya usalama katika eneo hilo.
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema Kituo cha Nyuklia cha Bushehr kimeingia miongoni mwa vituo 10 bora vya nyuklia duniani kwa mwaka wa tatu mfululizo baada ya kupata alama kamili ya 100/100 katika tathmini za kimataifa za usalama na ufanisi wa uendeshaji.