ubeberu
-
Katika ujumbe kwa Mkutano wa Mwaka wa Umoja wa Vyama vya Wanafunzi wa Kiislamu barani Ulaya; Kiongozi wa Mapinduzi:
Hitaji kuu la dunia leo ni mfumo wa haki wa kitaifa na kimataifa wa Kiislamu / Shambulio la Marekani lilishindwa mbele ya ujasiri wa vijana wa Iran
Ayatollah Khamenei, katika ujumbe wake kwa Mkutano wa 59 wa Mwaka wa Umoja wa Vyama vya Wanafunzi wa Kiislamu barani Ulaya, amesisitiza kuwa sababu kuu ya msukosuko na wasiwasi wa madhalimu wafisadi si suala la nyuklia, bali ni kuinuliwa kwa bendera ya kupinga mfumo usio wa haki na utawala wa mabavu wa mfumo wa ubeberu duniani, pamoja na mwelekeo wa Iran ya Kiislamu kuelekea kujenga mfumo wa haki wa kitaifa na kimataifa wa Kiislamu.
-
Mwakilishi wa Kiongozi wa Kidini katika Taasisi ya Mashujaa:
"Tutaendeleza vita dhidi ya ubeberu hadi bendera ya haki itakapoinuliwa juu"
Sheikh Hujjatul-Islam wal-Muslimin Musavi Muqaddam, Mwakilishi wa Kiongozi wa Kidini (Waliyyul-Faqih) katika Taasisi ya Mashujaa na Masuala ya Wapiganaji wa Kiislamu, amesema kuwa: "Tuna malengo makubwa, na kwa ajili ya kuyafikia tutaendelea kujitahidi na kusimama imara. Tutaendeleza vita dhidi ya ubeberu hadi pale bendera ya haki itakapoinuliwa na thamani za kibinadamu zitakapohifadhiwa."
-
Arubaini Iwe Sauti ya Umoja wa Kiislamu na Upinzani (Muqawamah) Dhidi ya Ubeberu na Uistikbari wa Kimataifa - Rais wa Waqfu Iran
“Arubaini ya mwaka huu inapaswa kuleta tumaini kwa Waislamu na kuwavunja nguvu maadui. Umoja ndiyo njia ya wokovu kwa Ulimwengu wa Kiislamu na Bendera ya Mapambano dhidi ya mfumo wa kishetani lazima ibaki juu.”