Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (AS) - Ibna - Hojjat-ul-Islam, Raja Nasser Abbas Jafari, Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan amelaani vikali shambulio la kinyama la kulipuliwa Ghaza na utawala wa Kizayuni kwa uungwaji mkono wa Marekani.
Akieleza kuwa damu za Waislamu wasio na hatia zimemwagwa huko Ghaza na nyumba zimeharibiwa, alisema: Haya yote si maafa ya eneo moja tu, bali pia ni alama ya kujiuliza juu ya dhamiri za Ummah mzima wa Kiislamu.
Rajah Nasser aliongeza: Kila siku apocalypse (zama za mwisho wa dunia) huwanyeshea Waislamu wa Palestina, na kila usiku ni giza, jambo ambalo linadhihirisha kutojali kwetu zaidi. Lakini tukio chungu zaidi si tukio la eneo la Gaza, bali ni ule ukimya unaojiri katika majumba (makasri) ya watawala wa Kiislamu na Kiarabu. Lugha ambazo wakati fulani zilizungumza kutetea Uislamu, leo zinashughulika kulamba nyayo za madola (mataifa) ya kibeberu. Mikono ambayo ilipaswa kuinuliwa kuelekea kuwasaidia wahitaji, leo hii inafanya harakati za kuishia kuelekea kwenye kutia saini na kuhitimisha mikataba ya biashara.
Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan aliendelea: Enyi watawala Waislamu na Waarabu! Ninyi ndio mna mali, rasilimali na ushawishi, lakini mioyo yenu imekufa. Macho yenu yamefungwa nandimi zenu zimekuwa ni bubu na heshima yenu imetoweka. Je, hamjui kwamba Mwenyezi Mungu hayuko pamoja na madhalimu?!. Mmesahau kuwa kukaa kimya ni sehemu ya dhulma (na uovu)? Ukimya wenu unasababisha hasira ya Mwenyezi Mungu. Qur'an inatukumbusha tena na tena ikisema:
«وَلاَ تَحْسَبَنَّ اللَّهَ غَافِلاً عَمَّا یَعْمَلُ الظَّالِمُونَ» / "Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayoyafanya madhalimu."
Seneta Rajah Nasser alisema: Akina Mama wa Gaza wanawavisha sanda watoto wao na nyinyi mnakaa nyuma ya meza zinazong'aa na kufanya (kusaini) mikataba ya kibiashara? Majeshi yenu yanashughulika na kazi ya kuwakandamiza watu wenu wenyewe, lakini hakuna hatua hata moja inayochukuliwa kwa ajili ya Palestina? Jua na tambueni kuwa wakati umekaribia ambapo ukimya huu utakuwa balaa kwenu na ardhi itatetemeka na hasira ya Mwenyezi Mungu itashuka juu yenu.
Mwishoni, alisema: Ni wakati wa kuamka (na kuwa macho). Bado kuna wakati wa kuunganisha mioyo, kusimama dhidi ya dhulma, na kusaidia wanyonge wanaodhulumiwa na kukandamizwa, vinginevyo siku ambayo historia itakuiteni, fedheha haitakuwa mbali.
Your Comment