Ulimwengu wa Kiislamu
-
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt(AS);
Amezisifu Mamlaka za Kidini na Wanazuoni wa Kiislamu / Kiongozi wa Mapinduzi ni kielelezo cha Elimu, Ucha Mungu, Kupinga dhulma, na Mamlaka ya Dini
Katika taarifa yake muhimu na ya kina, Katibu Mkuu wa Jukmuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (as) -ABNA - amelaani matusi na vitisho vya hivi karibuni dhidi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kushukuru misimamo yenye nuru ya viongozi na wasomi wakuu (Marajii) wa kidini duniani.
-
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu ya Ukaribu baina ya Madhehebu za Kiislamu: "Uhalifu wa Israel ni Jeraha kwenye Mwili wa Umma wa Kiislamu"
Hojjatul Islam Wal-Muslimeen Dakta Hamid Shahriari, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu ya Ukaribu baina ya Madhehebu za Kiislamu ameandika katika ujumbe wake kwenye Twitter yake kuwa: "Uhalifu wa Israel sio tu kuishambulia Iran, bali pia ni jeraha kwenye mwili wa Umma wa Kiislamu."
-
Habari iliyoenea ya ufunguzi wa Ofisi ya ABNA nchini Ghana katika Vyombo vya Habari nchini Ghana
Sambamba na ufunguzi wa Ofisi ya kikanda ya Shirika la habari la ABNA nchini Ghana, vyombo vya habari vya nchi hiyo vilikaribisha uwepo wa chombo hiki cha habari cha kimataifa na kukitambulisha kama jukwaa la kusambaza simulizi za kitamaduni na kidini kutoka ulimwengu wa Kiislamu hadi Afrika Magharibi.
-
Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Mahujaji: "Ulimwengu wa Kiislamu wahitaji kutekeleza mafundisho ya Hija ili kusitisha maafa ya Gaza"
Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa Ulimwengu wa Kiislamu kwa sasa unayahitaji zaidi kuliko wakati mwingine wowote mafundisho ya Hija, na akibainisha kuwa Hija ya mwaka huu ni msimu wa pili unaofanyika sambamba na jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza, ameuliza swali lifuatalo:“Ni nani anapaswa kusimama dhidi ya janga hili la kibinadamu?” Kisha ameongeza kwa kusisitiza: “Bila shaka yoyote, serikali za Kiislamu ndizo zinazobeba wajibu wa kwanza wa jukumu hili, na mataifa ya Kiislamu yana haki ya kudai utekelezaji wa wajibu huo kutoka kwa serikali zao.”
-
Palestina lazima ibaki / Watawala wetu wamepotoka kutoka kwenye Misingi ya Umma wa Kiislamu
Mwenyekiti wa Majlisi ya Umoja wa Waislamu wa Pakistan akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuiunga mkono Palestina amesema kuwa, watawala na wanasiasa wa sasa wa nchi hiyo wamejitenga na thamani halisi za Umma wa Kiislamu.
-
Mwenyekiti wa Bunge la Umoja wa Waislamu wa Pakistan:
Kila siku huko Gaza ni Apocalypse (Zama za Mwisho / Mwsiho wa Dunia) / Ukimya wa watawala wa Kiarabu unatia uchungu zaidi kuliko uhalifu (jinai)
Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan amesema: "Tukio chungu zaidi si tukio la uhalifu unaofanyika dhidi ya Gaza, bali ni kile kimya kinachojiri katika Kasri za watawala wa Kiislamu na Kiarabu." Lugha zilizokuwa zikizungumza kutetea Uislamu sasa hivi zinalamba nyayo za madola ya kibeberu.