Lugha
-
Araghchi Ahoji Jordan: Iran Isubiri Muda Gani Kabla ya Kujibu Uchokozi?
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amepinga madai ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan kwamba shambulio la Iran dhidi ya nchi za eneo lilikuwa si majibu kwa sababu lilitokea muda mfupi baada ya kuanza kwa mashambulizi ya Marekani, akisisitiza kuwa mashambulizi hayo yalitumia anga, ardhi na maji ya nchi za Kiarabu.
-
Qalibaf: Trump Alisaini Kutambua Kambi ya Upinzani (Muqawama)
Qalibaf amesema Donald Trump, wakati wa kusaini Mkataba wa Maelewano, alisaini pia utambuzi wa Kambi ya Upinzani kwa lugha ya Kiajemi, baada ya Marekani kutaka Iran iachane na makombora, harakati za Upinzani, mpango wa nyuklia na suala la Mlango wa Hormuz.
-
Ansarullah: Mabadiliko ya Kauli za Trump Yamesababishwa na Nguvu ya Uzuiaji ya Iran
Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kubadilika kwa kauli za Donald Trump kuelekea lugha ya amani kunatokana na kutambua hali halisi ya uwanja na uwezo wa Iran wa kuzuia vitisho vya kijeshi katika eneo hilo.
-
Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi: Marekani Inaelewa Zaidi Lugha ya Uchumi Kuliko Ahadi za Kisiasa
Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Mohammad Mokhber, amesema Iran haitakubali makubaliano yasiyotekelezwa kikamilifu na kusisitiza kuwa haki za wananchi wa Iran pamoja na damu za mashahidi haziwezi kusahaulika.
-
Sababu za Sayyid Ali Khamenei Kukubalika Hata Ndani ya Jamii za Wananchi wa Ulaya
Sayyid Ali Khamenei hakubaliki kwa sababu ya utaifa au dini tu, bali kwa sababu: 1_Anawakilisha kupinga dhulma. 2_Anaonekana kuwa na msimamo. 3_Na anazungumza lugha ya waliodhulumiwa ambayo huvuka mipaka ya dini na rangi.
-
Marekani na Israel Baada ya Kushindwa katika Vita vya Siku 12; Wanajaribu Kuchochea Ghasia Nchini Iran / Vyombo vya Habari Vihangaike Kutoa Ukweli
Baada ya kushindwa katika vita vya siku 12, Marekani na Israel wanajaribu kuhamishia shinikizo ndani ya Iran kwa kuchochea ghasia za kiuchumi na kijamii; wachambuzi wakisisitiza umuhimu wa vyombo vya habari kusambaza ukweli na kutofautisha kati ya madai halali na machafuko.
-
Jukumu la Marajii wa Kidini wa Kishia katika;
"Kulinda Umoja wa Kitaifa na Utambulisho wa Iran / Sehemu ya Saba: Kisa cha Kuokolewa kwa Lugha ya Taifa ya Iran na Ukombozi wa Azarbaijan"
Kulinda umoja wa ardhi na kuzingatia utambulisho wa kidini ni miongoni mwa masuala yaliyokuwa yakipewa umuhimu mkubwa na viongozi wa kidini katika ardhi za Kiislamu. Kiasi kwamba kila aina ya uvamizi au shambulio dhidi ya ardhi za Kiislamu ilikabiliwa na mwitikio mkali kutoka kwao. Uvamiuzi wa Azarbaijan wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na juhudi za kuutenga mkoa huo kutoka Iran ni miongoni mwa mambo yaliyodhihirisha tena ushawishi wa uongozi wa kidini katika kulinda umoja wa ardhi ya nchi. Aidha, kulinda utambulisho wa kitaifa wa Kiairani pia lilikuwa ni mojawapo ya masuala yaliyopatiwa umuhimu maalum na viongozi (Marajii) wa kidini katika kipindi cha utawala wa Pahlavi.
-
Sisi na wamagharibi kwa Mtazamo wa Imam Khamenei – Mkutano Uliofanyika Nchini Kenya +Picha
Pourmarjan: “Ayatollah Khamenei, kama mwanafiqhi na mwanafikra mashuhuri katika ulimwengu wa Kiislamu, na ambaye ametumia zaidi ya miaka sitini katika nyanja za kielimu, kidini, kitamaduni, na kisiasa, ametoa mitazamo sahihi na ya kimkakati kuhusu Magharibi. Uelewa wa fikra hizi ni muhimu sana kwa kizazi cha leo cha vijana na wasomi.”