Mwanachama wa kitengo cha habari cha timu ya mazungumzo ya Iran amesema kuwa hakuna ukaguzi wowote utakaofanyika katika vituo vya nyuklia vilivyoharibiwa na vita, huku akisisitiza kuwa maamuzi kuhusu vikwazo na suala la nyuklia yatafanywa baada ya utekelezaji wa Kifungu cha 13 cha hati ya maelewano.
Mwakilishi wa Urusi mjini Vienna amesema wito wa nchi za Magharibi wa kurejesha mara moja ukaguzi wa vituo vya nyuklia vya Iran hauna uhalali, akieleza kuwa hatua za Marekani na washirika wake ndizo zilizochochea hali ya sasa.
Vikosi vya kikoloni vilivamia maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi usiku wa jana na asubuhi ya leo, na kufanya ukaguzi wa nyumba za baadhi ya waliokuwa mateka waliotolewa huru.