Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetoa onyo kwamba mtu, kituo au eneo lolote litakalotoa msaada kwa vikosi vya Marekani katika mashambulizi dhidi ya Iran litachukuliwa kuwa lengo halali la vikosi vya Iran.
Marais wa Benki Kuu za Iran na Urusi wamehimiza kuimarishwa kwa ushirikiano wa kifedha, kupanuliwa kwa biashara baina ya nchi hizo mbili, na kuendelezwa kwa Mradi wa Ukanda wa Kaskazini (North Corridor) ili kurahisisha miamala ya kiuchumi.
Kamanda wa Kikosi cha Quds katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ismail Qaani, amesema kuwa hatua za wakati muafaka na za “busara” zinazochukuliwa na Yemen zinaonyesha uimara na mshikamano wa mhimili wa Muqawama. Amesema pia kuwa, endapo kutahitajika, pande nyingine zinaweza kujiunga katika hatua hizo.