Yedioth Ahronoth: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran bado ni miongoni mwa wachezaji wachache wa eneo hili wanaomiliki nguvu halisi ya kuzuia mashambulizi — uwezo ambao licha ya hasara za hivi karibuni, haujapungua bali unaimarika na kufafanuliwa upya.
Shirika la Redio na Televisheni la utawala wa Kizayuni limedai kwamba Misri, sambamba na kuongezeka kwa operesheni za kijeshi za Israel huko Gaza, imetuma maelfu ya wanajeshi na vifaa vya kijeshi katika eneo la kaskazini mwa Jangwa la Sinai lililoko mpakani na Ukanda wa Gaza na Israel.