Ayatollah Al-Udhma Abdullah Javadi Amoli alisisitiza umuhimu wa kuunganisha sanaa na ushairi na Tauhidi (umoja wa kumpwekesha Mwenyezi Mungu), akisema kuwa iwapo mafundisho ya tauhidi yatahuishwa kwa sura yake halisi, basi jamii ya Kiislamu haitapotea wala kukumbwa na vitisho kutoka kwa maadui.
Washairi wa Kiislamu kutoka sehemu mbalimbali watahudhuria kwa ajili ya kusoma mashairi yanayogusa nyoyo kuhusu: Tukio la Ghadir, Mapenzi kwa Ahlul-Bayt(as), na mafundisho ya Kiislamu.
Washairi Mashuhuri wa Kishia na Kisunni kutoka maeneo yote ya Kurram wamekusanyika katika tamasha lenye mada ya amani lililofanyika katika mji wa Parachinar, Pakistan.