Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Saeed Khatibzadeh, amesema kile alichokiita “mhimili wa kigaidi” kimeshindwa kufikia malengo yake dhidi ya Iran, akisisitiza kuwa Tehran imeazimia kuwawajibisha wahusika wa vitendo vya kigaidi dhidi ya nchi hiyo.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kufungwa kwa muda kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz, likisema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kile lilichodai kuwa ni ukiukaji wa maelekezo ya usalama wa baharini na kuendelea kwa uingiliaji wa mataifa ya kigeni katika eneo hilo.
Mkuu wa Mamlaka ya Mahakama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Marekani na utawala wa Kizayuni zimetenda uhalifu wa kivita dhidi ya Iran na wananchi wake, akisisitiza kuwa wahusika watafuatiliwa kisheria, wataadhibiwa na kulipa fidia inayostahili.