Taarifa iliyotolewa na mamlaka za Uganda imesema sababu ya ajali hiyo ya moto iliyotokea usikuwa kuamkia leo haijajulikana, lakini vyombo vya usalama vimeanzisha uchunguzi wa kubaini chanzo chake.
Habari zaidi zinasema kuwa, watu wengine sita wamelazwa katika Hospitali ya Herona mjini Kisoga kutokana na majeraha ya kuungua kwenye tukio hilo.
Waziri wa Masuala ya Walemavu wa Uganda, Hellen Grace Asamo amesema yumkini idadi ya vifo na majeruhi ni kubwa kutokana na mabweni ya shule hiyo kuwa na vizuizi vya chuma kinyume na sheria.
Matukio ya ajali za moto katika shule za Uganda yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Mwezi Machi mwaka huu, Wizara ya Elimu ya Uganda ilisema ajali hizo zinaripotiwa mara kwa mara kutokana baadhi ya taasisi hizo za elimu hususan za binafsi kuendeshwa bila leseni na vibali kutoka mamlaka husika.
Baadhi ya wazazi wakiondoka shuleni na wanaoMwaka 2008, wizara hiyo kwa ushirikiano na polisi ya Uganda ilitoa orodha ya mambo yanayopaswa kufuata ili shule za nchi hiyo ziweze kuondokana au kudhibiti ajali hizo za moto.
Baadhi ya maelekezo hayo yaliyotolewa na Wizara ya Elimu ya Uganda ni pamoja na kuzitaka shule kuweka malango ya dharura, kuunda kamati za usalama na kuwa na vifaa vya kuzima moto shuleni. Hata hivyo makumi ya watu wameendelea kuaga dunia katika mikasa ya moto shuleni nchini Uganda licha ya mikakati hiyo ya serikali.
342/