Waziri Mkuu Najib Mikati anasema alikuwa na nia ya kusafiri kwenda New York kushiriki katika mkutano Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lakini aliamua kutosafiri baada ya matukio ya wiki hii. "Ninasisitiza kwamba hakuna kipaumbele kwa sasa ambacho ni cha juu zaidi kuliko kukomesha mauaji yanayofanywa na adui - Israel na aina mbalimbali za vita wanavyoendesha," ilisema taarifa hiyo.
"Pia natoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na ulimwengu kuchukua msimamo wa wazi kukabiiliana na mauaji haya ya kutisha."
Mikati pia anatoa wito wa "kupitishwa kwa sheria za kimataifa ili kupunguza njia za kiteknolojia za kiraia kutoka kwa malengo ya kijeshi na vita" kutokana na mashambulizi ya vifaa vya mawasiliano nchini mwake.
Wakati huo huo, Harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imevurumisha msururu wa makombora ya kulipiza kisasi dhidi ya makao makuu ya kijasusi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kambi za kijeshi za utawala huo baada ya mashambulizi ya anga ya Israel kwenye mji mkuu wa Lebanon, Beirut.
Mashambulio hayo yamefanyika baada ya jeshi la Israel kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya mji mkuu wa Lebanon, na kuua takriban watu 14 na kujeruhi wengine zaidi ya 59. Aghalabu ya waliouawa walikuwa watoto na wanawake waliokuwa katika jengo la raia mjini Beirut. Aidha Ibrahim Aqil mmoja wa makamanda wakuu wa Hizbullah ni miongoni mwa waliouawa shahidi katika shambulio hilo la Israel.
342/