Akijulikana kwa juhudi zake katika kujenga ushirikiano wa Dini mbalimbali, Suleiman aliwahi kuwa mpatanishi wakati wa mgogoro wa kutekwa kwa Sinagogi la Colleyville 2022 na alitambuliwa na kuthaminiwa na Baraza la Wawakilishi la Texas kwa juhudi zake.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), Suleiman alilaani usambazaji wa maudhui "hatari" na "yasio na maadili" uliofanywa na Bilionea huyo.
Alisema: "Gari la Tesla linapopata ajali, mara moja unalaani kwa uonevu vyombo vya Habari. Lakini kwa muda wa wiki nzima, umekuza na kueneza kila dhana potofu inayowezekana kufikirika dhidi ya Uislamu."
Suleiman pia alipendekeza kuwa mazungumzo ya kujenga (na yenye manufaa) yafanyike na Mkurugenzi Mtendaji wa Tesla.
Ukosoaji huo ulikuja baada ya Musk kuingilia kati kwenye utata katika mijadala ya Uingereza kuhusu "Magenge ya ulaghai", ambapo yeye alisisitiza asili ya Pakistan na ya Kiislamu ya baadhi ya washukiwa na kupuuza takwimu rasmi kutoka katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza.
Kwa mujibu wa takwimu hizi, asilimia 88 ya wahalifu katika visa hivyo ni wazungu, huku asilimia 7 pekee wakiwa ni Wa_Asia.
Musk, ambaye huenda akawa mshauri wa Mambo ya Nje wa utawala ujao wa Trump, pia anajulikana kwa mashambulizi yake dhidi ya Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na wito wake wa "Ukombozi" wa watu wa Uingereza kutoka kwa "Serikali Dhalimu" ya nchi hiyo.
