19 Machi 2025 - 18:25
Source: Parstoday
Iran imeuza madini yenye thamani ya dola bilioni 12 katika kipindi cha mwaka mmoja

Mauzo ya nje ya madini ya Iran yameongezeka katika miezi 11 ya mwaka wa Kiirani hadi mwishoni mwa Februari, yakifikia jumla ya dola bilioni 12.599.

Takwimu zilizotolewa na Shirika la Habari la IRIB zinaonyesha kuwa Iran iliuza nje zaidi ya tani milioni 58.5 za bidhaa za madini na metali katika miezi 11 ya kwanza hadi Februari 18.

Ripoti ya IRIB imebaini kuwa takwimu hizi zinaonyesha ongezeko la asilimia 1.2 kwa thamani na asilimia 0.4 kwa kiasi ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Aidha taarifa hiyo imebaini kuwa mauzo ya nje ya chuma, aluminium na shaba yaliwakilisha thamani ya dola bilioni 9.821 kati ya mauzo ya nje ya madini na metali ya Iran katika kipindi cha Aprili hadi Februari, ikieleza kuwa usafirishaji wa metali hizo tatu ulifikia karibu tani milioni 31.5.

Mafanikio hayo yamefikwia pamoja na kuwa wazalishaji wa chuma wamekuwa wakikumbwa na uhaba wa nishati mwaka huu wa kalenda katikati ya ongezeko la mahitaji ya umeme na gesi asilia katika sekta za nyumba na biashara za Iran.

Hii inakuja wakati kampuni ya serikali ya shaba ya Iran iliporipoti ongezeko kubwa la mauzo yake ya kimataifa katika miezi 10 ya kalenda hadi Januari 19, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo mapema Februari ikionyesha kuwa mauzo ya nje yaliongezeka kwa asilimia 956 kwa thamani ya dola, yakifikia sawa na dola milioni 644.

Kulingana na Shirika la Maendeleo la Migodi na Viwanda vya Madini la Iran, ripoti ya hivi karibuni kutoka kwa Chama cha Dunia cha Chuma (World Steel Association) inaonyesha kwamba Iran inashika nafasi ya 10 duniani kana mzalishaji wa chuma.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha