Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-: Samahat Sheikh Musabaha Mapinda, akitoa Salam za Rambirambi katika Mazishi ya Marhuma Ukhti Fatima Mwiru amesema:
"Nimemfahamu Fatima Mwiru zaidi ya Miaka 20 iliyopita katika Harakati mbali mbali za Kidini.
Dada Fatima ana upekee wake, Kwanza ni katika Wasomi wetu wa Mwanzo kwa upande wa kina Mama Nchini Tanzania.
Lakini pia, ni Mwanamke wa kupigiwa mfano katika Jamii, Mpambanaji kwa ajili ya Dini, aliyefanikiwa katika Maisha yake kuasisi Kituo cha Kidini chenye kutoa na kusambaza Maarifa ya Kiislamu. Katika athari zake nzuri ni kuacha Msikiti ambao ulipatikana kutoka juhudi na Harakati zake za Kidini.
Kama Waislamu wa Tanzania na kama Wapenzi na Wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s), tumepoteza mtu muhimu Sana katika Uwanja wa Tabligh.
Your Comment