4 Aprili 2025 - 23:42
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl al-Bayt (A.S) akutana na Msimamizi wa Atabat Hosseini | Tangazo la utayari wa kushirikiana kiutamaduni

Ayatollah "Reza Ramezani" alikutana na Hojjat al-Islam na Waislamu Sheikh "Abdul Mahdi Karbalai".

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna - Ayatollah "Reza Ramezani" na ujumbe alioambatana nao walikutana na Hojjat-ul-Islam wal- Muslimina Sheikh "Abdul Mahdi Karbalai", Msimamizi wa kisheria wa  Atabat Hosseini, alipozuru Haram Tukufu ya Imam Hussein (a.s) akiwa safarini katika Mji wa Karbala. Katika mkutano huu, kulikuwa na majadiliano na kubadilishana mawazo kuhusu shughuli za Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS) na kushirikiana katika programu za pamoja kati yaJumuiya hii na Atabat Hosseini.

Katika mkutano huu, Ayatollah Ramezani alikutana na Hojat al-Islam "Mohammed Ali Muinian", Makamu / Msaidizi wa Masuala ya Kimataifa ya Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl al-Bayt (AS), Hojjat al-Islam "Syed Muhammad Reza Al-Ayoub", Mkurugenzi wa Ofisi ya Mwakilishi wa Jumuiya ya Ahlu al-Bayt (AS) nchini Iraq, "Hassan Khokirand", Mshauri wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlu al-Bayt (AS) kwa masuala ya nchi za Kiafrika na Kiarabu, na Dkt. Sayyid Muhsin Aali Batul (A.S) Profesa wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Ahl al-Bayt (AS) ambaye alifuatana nao.

Mwanzoni mwa mkutano huu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlu al-Bayt (AS) alipokuwa akitoa pongezi za mnasaba wa Siku ya Eidul-Fitr kwa Msimamizi wa kisheria wa Atabat Hosseini, aliwasilisha ripoti kuhusu programu za hivi karibuni za Jumuiya hii na hatua zake za kuleta mabadiliko katika nyanja za Elimu, Tabligh na Utamaduni katika uga wa Kimataifa.

Katika ripoti yake, alitaja mahususi shughuli za kimisionari (kitablighi) za wajumbe na Wamisionari (Mubalighina) wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS) , Shirika la Habari la Abna, Chuo Kikuu cha Ahl al-Bayt (a.s), Mtandao wa Satelaiti wa Thaqalayni, Wiki Shia, na vijitabu na vitabu vilivyotafsiriwa katika mkusanyiko huu.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl al-Bayt (A.S) akutana na Msimamizi wa Atabat Hosseini | Tangazo la utayari wa kushirikiana kiutamaduni

Akiendelea na mkutano huu, Ayatollah Ramezani ametoa shukurani za pekee kwa Atabat Hosseini kwa ushirikiano wake na Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS) katika kufanya mikutano na makongamano maalumu ya Jumuiya hii katika siku za Arbaeen ya Hosseini mwaka 2024 huko Karbala, amezungumzia mafanikio ya mikutano na makongamano hayo, na ametoa wito wa kuendelea na maingiliano na ushirikiano zaidi kwa ajili ya maendeleo na mafanikio ya Arobaini ya mwaka huu.

Hojjat al-Islam wa Muslimin Sheikh "Abdul Mahdi Karbalai", Msimamizi wa Sharia wa Atabat Hosseini, baada ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl al-Bayt (AS) na Ujumbe aliofuatana nao, alitangaza utayari kamili wa Atabat Hosseini kushirikiana na kuamiliana na Jumuiya ya Kimataifa ya Kitamaduni za Ahl al-Bayt (a.s) wakati wa kufanya programu za pamoja za kitamaduni za Ahlul-Bayt (AS) katika Siku za Arbaeen na siku zingine za mwaka.

Mwishoni mwa mkutano huu, Hojjat al-Islam Al-Ayoub, Mkurugenzi wa Ofisi ya Mwakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (AS) nchini Iraq, aliwasilisha ripoti ya shughuli za Jumuiya hii nchini Iraq kwa Msimamizi wa Sharia ya Atabat Hosseini.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl al-Bayt (A.S) akutana na Msimamizi wa Atabat Hosseini | Tangazo la utayari wa kushirikiana kiutamaduni

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha