8 Aprili 2025 - 20:04
Source: Parstoday
Maandamano ya kumpinga Trump yamesababishwa na mambo mengi

Huku wananchi wa Marekani wakiendelea kukasirishwa na siasa za kidikteta na uingiliaji kati za Trump, Elon Musk na serikali yao, wataalamu wanasema kuna sababu nyingi zilizopelekea mamia ya maelfu ya watu wajitokeze kote Marekani na nje ya Marekani kupinga siasa za Washington.

Jana Jumatatu jarida la Marekani la Newsweek liliripoti kupamba moto maandamano katika kona zote za Marekani kupinga siasa za Trump na kusema: Maandamano ya taifa zima yaliyobebwa na kaulimbiu ya "Hands Off" (yaani acha uingiliaji) dhidi ya utawala wa Trump yamefanyika si tu katika majimbo yote 50 ya Marekani, Washington, D.C na Puerto Rico, bali pia katika nchi nyingi nje ya Marekani.

Jarida la Newsweek limeandika: Watu wameshiriki katika maandamano hayo kwa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kupinga kashfa ya "Signalgate" (kuvujisha habari kuhusu mashambulizi ya anga nchini Yemen), kuvamiwa wahamiaji kwenye vyuo vikuu na kutozwa ushuru mpya wa kiuchumi.

Jarida hilo pia limeandika: Maandamano hayo yameonesha kuwa idadi kubwa ya Wamarekani hawaridhishwi na namna Trump anavyoendesha serikali. Pia hawaridhishwi na utawala wa Trump - hasa kuweko Elon Musk katika Idara ya Ufanisi wa Serikali (DOGE) - na wanaamini kuwa hayo ni miongoni mwa mambo ambayo yamewafanya Wamarekani wakasirike na waamue kumiminika kwa mamilioni mitaani kumpinga Trump na serikali yake. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, maandamano ya "Hands Off" yamefanyika pia katika miji ya Vienna, Austria, miji ya Lyon, Nice na Paris huko Ufaransa, Miji ya Berlin na Frankfurt ya Ujerumani, mji wa Guadalajara wa Mexico, Amsterdan, Uholanzi, Lisbon, Ureno na London Uingereza.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha