8 Aprili 2025 - 20:06
Source: Parstoday
Wanamitandao wa Iran: "Trump anasema uwongo", "Marekani Shetani hatoki hatiani kwa mazungumzo"

Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa X wametuma jumbe mbalimbali za kukosoa sera za Rais wa Marekani dhidi ya Iran na ushirikiano wake na viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika kufanya jinai za kivita huko Ghaza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araghchi ameandika katika ujumbe kwenye akaunti yake ya X: "Iran na Marekani zitakutana nchini Oman siku ya Jumamosi kwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja katika ngazi ya maafisa wakuu".

Karibuni hivi, Rais wa Marekani Donald Trump amedai kuwa Iran itafanya mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani. 

Kwa mujibu wa Pars Today, baadhi ya watumiaji wa Iran wa mtandao wa X wametuma jumbe kadhaa kujibu madai hayo ya rais wa Marekani.

Navid Mostafeizi, mtumiaji wa Kiirani wa mtandao wa X ameandika: "Maneno ya maafisa wa nchi yangu kuhusu mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani ni ya kuaminika zaidi kwangu mimi kuliko madai ya Trump kuhusu mazungumzo ya moja kwa moja. Shetani mcheza kamari anaendesha vita vya kisaikolojia na habari zisizo na uhakika ili kuzusha mpasuko na kuulenga utulivu, maisha na uchumi wa Iran".

Mwanaharakati wa kisiasa nchini Iran Hamid Rasaei yeye amesema: "wakati Janabi Araghchi anazungumzia kuanza mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani ifikapo Jumamosi, Trump anadai kufanyika mazungumzo ya moja kwa moja kuanzia Jumamosi! Anasema uwongo, kwa sababu ahadi yake ya kumaliza vita vya Ukraine na mapigano kati ya Hamas na Israel haijatekelezwa; anahitaji mafanikio ya haraka ya kidiplomasia ili kushinda vita vyake vya ushuru".../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha