Rais Pezeshkiana alisema hayo jana na kusisitiza kuwa: "Tuna imani na mazungumzo, lakini si chini ya udhalilishaji. Tunafanya mazungumzo na dunia nzima na hatuna ugomvi na mtu yeyote, lakini hatutamnyenyekea mtu na hatufanyi mazungumzo kwa gharama yoyote tu. Hatutaki vita wala machafuko na wala mabomu ya nyuklia. Sijui dunia inataka tuithibitishie nini tena?
Aidha amesema: "Wakati wa sherehe za Sikukuu ya Idul Fitr niliwasiliana na kufanya mazungumzo ya simu na viongozi wa nchi zote za eneo hili. Uhusiano wetu hivi sasa na nchi zote hizi ni mzuri sana. Lakini suala la mazungumzo na Marekani ni kitu kingine. Wakati nchi kama Marekani inapotuwekea vikwazo na mashinikizo ya pande zote na kila siku inatoa vitisho dhidi yetu, vipi itawezekana kufanya mazungumzo na nchi kama hiyo?"
Kwa mara nyingine tena Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitizia msimamo usiotetereka wa Tehran wa kutoanzisha vita na nchi yoyote na wakati huo huo iko imara kwa ajili ya kujihami na kuongeza kuwa: "Sisi tumeshauthibitishia ulimwengu kuwa hatutaki vita, hatutaki bomu la nyuklia na hatutaki machafuko, bali tunataka utulivu. Hivi sasa ni zamu ya Wamarekani wathibitishe kivitendo kuwa kweli wanataka mazungumzo. Suala la kwamba Iran haitaki silaha za nyuklia si maneno ya Tehran tu, bali hiyo ni Fatwa ya Kidini ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambayo ni wajibu kutekelezwa.
342/
Your Comment