8 Aprili 2025 - 20:08
Source: Parstoday
Ndege za kivita za Marekani zashambulia Yemen karibu mara 30 katika muda wa chini ya siku moja

Marekani imefanya karibu mashambulizi 30 ya anga katika majimbo kadhaa kote nchini Yemen katika muda wa chini ya siku moja, na kushadidisha uchokozi wake dhidi ya taifa hilo, katika kile ambacho wataalamu wamekitaja kuwa ni harakati za kujishinda yenyewe za kusitisha bila mafanikio operesheni za Sana'a zinazotekelezwa dhidi ya Israel na waungaji mkono wake kwa ajilii ya kuwatetea wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.

Kwa mujibu wa duru za Yemen, ndege za kivita za Marekani zimefanya mashambulizi 11 ya anga katika mkoa wa Sana’a leo Jumanne, yakilenga zaidi wilaya za Bani Hushaysh na Sanhan.Mashambulizi ya mabomu na makombora yailienea zaidi mashariki, huku 13 yakiripotiwa katika mkoa wa Ma'rib, ikiwa ni pamoja na wilaya za Majzar na Jawba.

Aidha, mashambulizi manne ya anga ya ndege za kivita za Marekani, yamefanywa dhidi ya Kisiwa cha Kamaran katika pwani ya mkoa wa al-Hudaydah magharibi mwa Yemen.Hayo yametajwa kama moja ya mashambulizi makali zaidi ya mabomu na mkombora yaliyofanywa katika moja wa siku moja na majeshi ya Marekani dhidi ya Yemen katika kipindi cha wiki za hivi karibuni.

Marekani inadai kuwa, mashambulizi yake yanalenga kudhoofisha uwezo wa kijeshi wa Yemen, hasa vitengo vya makombora na ndege zisizo na rubani vya nchi hiyo.Tangu Oktoba 2023 baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuanzisha vita vya kinyama na mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Ghaza, Vikosi vya Ulinzi vya Yemen YAF vimekuwa vikitekeleza operesheni nyingi dhidi ya maeneo yenye uhusiano na Israel kama njia ya kuulazimisha utawala huo wa Kizayuni usimamishe vita na kuondoa mzingiro dhidi ya Ghaza.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Yemen, mashambulio yanayofanywa na Marekani yamekuwa yakilenga maeneo ya kiraia tu na kugharimu maisha ya makumi ya watu wasio na hatia.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha