15 Aprili 2025 - 22:13
Source: Parstoday
Gazeti la US Today: Uchumi wa Marekani umekwama au unakaribia kwenye mdororo

Gazeti la US Today la Marekani limeandika kuwa utabiri unaonyesha kuwa ukuaji uchumi wa Marekani utakabiliwa na mkwamo au unakaribia kudorora licha ya kusimamishwa kwa ushuru wa Trump.

Gazeti hilo limeandika: Wachambuzi wa masuala ya uchumi wanatabiri kuwa uchumi wa Marekani utakabiliwa na mustakbali mbaya kutokana na vita vya kibiashara vilivyoanzishwa na Rais wa nchi hiyo, Donald Trump dhidi ya nchi nyingine duniani. 

Utabiri huu umetolewa licha ya Trump kusitisha kwa siku 90 tozo zake za ushuru ziada kwa nchi zaidi ya 50. 

Wakati huo huo Taasisi ya Walters Clover imetabiri kwa mujibu wa utafiti wa wachumi 46 kati ya Aprili 4 na 7 mwaka huu kwamba, uchumi wa Marekani utadorora mwaka huu 2025 kufuatia kukua kwa asilimia 0.8% pekee. Mwezi uliopita, utabiri ulionyesha kuwa uchumi wa Marekani ungekuwa kwa asilimia 1.7.

Tabiri nyingine zinaonyesha kuwa upo uwezekano uchumi wa Marekani ukadorora kwa asilimia 47. Mwezi Februari mwaka huu uchumi wa Marekani ulitabiriwa kudodora kwa asilimia 25.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha