19 Aprili 2025 - 20:39
Source: Parstoday
Press TV: Duru ya pili ya mazungumzo ya Iran na Marekani imefanyika Rome katika 'anga chanya'

Duru ya pili ya mazungumzo ya nyuklia yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani imefanyika katika mji mkuu wa Italia, Rome leo Jumamosi katika "anga chanya". Hayo yameelezwa na ripota wa chaneli ya televisheni ya Press TV.

Akiripoti kutoka nje ya ukumbi, Gisoo Misha Ahmadi, aliyefuatana na ujumbe wa Iran huko mjini Rome, ameripoti mubashara kuhusu mazungumzo hayo yaliyofanyika wiki moja baada ya duru ya kwanza ya mazungumzo iliyofanyika katika mji mkuu wa Oman, Muscat.

Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, IRIB limeripoti kuwa, kufuatia kile kilichoelezwa kama mazungumzo ya kujenga yaliyofanyika mjini Rome, kuna muelekeo mkubwa kwa wajumbe wa Iran, Marekani na Oman kufanya duru ya tatu ya mazungumzo hayo ndani ya kipindi cha siku chache zijazo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi na Steve Witkoff, mjumbe maalumu wa rais wa Marekani katika masuala ya Mashariki ya Kati, leo waliongoza mazungumzo ya ngazi ya juu yaliyofanyika kwa uratibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Badr bin Hamad Al Busaidi. Mazungumzo hayo yalifanyika kwa muda wa zaidi ya masaa manne.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baghaei amesema, mazungumzo hayo yasiyo ya ana kwa ana yalifanyika katika makazi ya balozi wa Oman mjini Rome na katika kumbi mbili tofauti.

Ameongeza kuwa Iran ilishiriki katika mazungumzo ya uondoaji vikwazo "kwa uzito na utayari kamili" na itaendelea kutoa ushirikiano mradi tu mazungumzo hayo yaendelee kuwa na nia ya kujenga.

"Mpango wa nyuklia wa Iran ni wa amani kabisa, na Iran iko tayari kuondoa mashaka yoyote yaliyopo katika suala hili," ameeleza Baghaei.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameendelea kueleza kwamba msimamo "thabiti na wa kimsingi" wa Iran uliobainishwa wakati wa mazungumzo na Marekani ni kutaka iondolewe vikwazo "haramu" ilivyowekewa kwa njia ya kuaminika na kwa mahakikisho yote yanayolazimu.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha