Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti kutokea tukio hatari la kiusalama kwa jeshi la Kizayuni kwenye Ukanda wa Ghaza ambalo limelilazimisha jeshi vamizi la Israel kutumia helikopta kuhamisha maiti na majeruhi.
Duru za utawala wa Kizayuni zimethibitisha habari hiyo na kusema, wanajeshi hao wa Israel wameuawa kwenye mashambulizi makali ya Muqawama dhidi ya wanajeshi wa Israel katika kitongoji cha Al-Tuffah mashariki mwa mji wa Ghaza.
Vyombo vya habari vya lugha ya Kiebrania vimefichua kwamba kwa uchache afisa mmoja wa Israel ameangamizwa na takriban wengine watano wamejeruhiwa wakati gari la kivita la Israel liliporipuliwa na Muqawama mashariki mwa Ghaza.
Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti pia kuwa, helikopta za Israel zimetumika kusafirisha wanajeshi waliojeruhiwa kutoka Ukanda wa Ghaza, baadhi yao wakiwa wamejeruhiwa vibaya.
Mtandao wa habari wa Hadashot wa utawala wa Kizayuni nao umeripoti kuwa mwanajeshi mmoja wa Israel amejeruhiwa katika mapigano na makundi ya Muqawama kwenye Ukanda wa Ghaza. Mwanajeshi huyo wa Israel amejeruhiwa vibaya kiasi kwamba helikopta za Israel zimelazimika kutumika kusafirisha majeruhi hao akiwemo mwanajeshi huyo.
Habari sahihi kuhusu operesheni hiyo na idadi hasa ya wanajeshi wa Israel walioangamizwa na kujeruhiwa haijapatikana kutokana na utawala wa Kizayuni kuchuja mno habari zinazohusiana na maafa inayopata huko Ghaza.
342/
Your Comment