10 Juni 2025 - 00:04
Ripoti ya IBN TV AFRICA: Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as)-ABNA- Yazindua Ofisi ya Kanda Afrika Magharibi Mjini Accra, Ghana + Video

Shirika la Habari la ABNA, ambalo kwa sasa linafanya kazi katika lugha 27, linajihusisha na kusambaza habari za kitamaduni na kidini kwa kiwango cha kimataifa. Miongoni mwa lugha zinazotumika ni pamoja na Kiingereza, Kifaransa, Kihausa, Kiswahili, Kiarabu, Kihispania, na Kireno.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Ibn Tv Africa katika ripoti yake juu ya tukio muhimu la Shirika la Habari Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- lililojiri huko  Accra, Ghana imesema: Katika hafla maalumu iliyojaa hadhira ya watu kutoka nyanja mbalimbali za kitamaduni, kidini na waandishi wa habari, ofisi ya kanda ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- kwa ajili ya Afrika Magharibi imezinduliwa rasmi mjini Accra, Mji Mkuu wa Ghana.

Ripoti ya IBN TV AFRICA: Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as)-ABNA- Yazindua Ofisi ya Kanda Afrika Magharibi Mjini Accra, Ghana + Video

Ofisi hiyo mpya inatarajiwa kuwa kituo muhimu cha usambazaji wa habari kwa mataifa ya Afrika Magharibi, ikilenga kuimarisha upashanaji wa taarifa na maadili ya kiroho, utu, na haki kupitia mtazamo wa Kiislamu unaotegemea mafundisho ya AhlulBayt (as).

Shirika la Habari la ABNA, ambalo kwa sasa linafanya kazi katika lugha 27, linajihusisha na kusambaza habari za kitamaduni na kidini kwa kiwango cha kimataifa. Miongoni mwa lugha zinazotumika ni pamoja na Kiingereza, Kifaransa, Kihausa, Kiswahili, Kiarabu, Kihispania, na Kireno.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi, Ayatollah Reza Ramazani, Katibu Mkuu wa Baraza la Dunia la AhlulBayt (as), alieleza umuhimu wa maadili ya juu katika uandishi wa habari. Alisema:

"Mtazamo wa kimantiki, wa kiroho, wa utu, na unaozingatia haki lazima utawale utangazaji wa habari wa ABNA."

Ripoti ya IBN TV AFRICA: Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as)-ABNA- Yazindua Ofisi ya Kanda Afrika Magharibi Mjini Accra, Ghana + Video

Hafla hiyo imepokelewa kwa furaha na matumaini makubwa na viongozi wa jamii, wanahabari, na waumini, kama hatua chanya kuelekea kuimarisha mawasiliano ya kiutamaduni na kidini katika bara la Afrika.

Ripoti ya IBN TV AFRICA: Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as)-ABNA- Yazindua Ofisi ya Kanda Afrika Magharibi Mjini Accra, Ghana + Video

Your Comment

You are replying to: .
captcha