Katika ujumbe alioutuma kwa Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), Sheikh Abdul Fattah Taruti amebainisha mshikamano wake na taifa adhimu la Iran wakati huu wa kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unaendeleza mashambulizi ya kichokozi dhidi ya Iran.
Sheikh Taruti katika ujumbe wake ameomba dua ya ushindi kutoka kwa Allah kwa taifa la Iran kupitia Baraka za Qur’ani Tukufu. Akilihutubu taifa la Iran amesema: “Wamisri pamoja na viongozi wao wako pamoja nanyi, wanawaunga mkono yote ambayo mnafanya dhidi ya adui Mzayuni aliyeanzisha hujuma.”
Sheikh Taruti aidha ametangaza mshikamano na watu wa Iran katika mapambano yao dhidi ya utawala ghasibu wa Israel kwa kusoma aya za Sura an-Nasr kama ilivyo katika klipu hii hapa chini.
342/
Your Comment