Balozi Iravani amesema kuwa mazungumzo yana kanuni zake, na ni mchakato wa kutoa na kupata. Kwa hivyo tunapaswa kushiriki katika mazungumzo na kujadiliana, labda tufikie hitimisho au la, lakini kusalimu amri bila masharti sio mazungumzo.
Ameongeza kuwa, Tutakuwa tayari kufanya mazungumzo kama Washington kweli inataka kufanya mazungumzo, lakini kama inataka kututishwa sera zake ni vigumu kufanya mazungumzo yoyote na nchi hiyo.
Balozi Saeid Iravani amelaani na kutaja hatua ya Rais Donald Trump ya kutishia kumuua Ayatollah Sayyid Ali Khamenei Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na kusema: Wakuu wa nchi wana kinga dhidi ya shambulio lolote kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa pia ametilia mkazo kuhusu haki ya Iran ya kurutubisha madini ya urani kwa mujibu wa mkataba wa NPT na kusema: Miradi ya Iran ya kurutubisha urani haitasimama hata baada ya hujuma ya mashambulizi ya Marekani dhidi ya taasisi za nyuklia za nchi hii.
342/
Your Comment