Amesema katika barua aliyomwandikia Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba: "Tunaomba kwa dhati Baraza la Usalama liutambue utawala wa Israel na Marekani kama waanzilishi wa uvamizi na wanaobeba dhima ya hujuma hiyo."
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia linapasa kuziwajibisha pande vamizi na kuzuia kujiri tena jinai ya kikatili na kubwa kama hiyo ili kudumisha amani na usalama duniani.
Sayyid Abbas Araqchi amesisitiza kuwa viongozi wa kisiasa na kijeshi wanaoagiza kutekelezwa hujuma za uvamizi pia wanabeba dhima kwa jinai ya kimataifa ya kuanzisha vita kwa mujibu wa sheria za kimataifa."
Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Iran ametaja hujuma ya mashambulizi ya Israel na Marekani kama “shambulio la kinyama” kwa mujibu wa sheria za kimataifa na kutahadharisha kuwa, kufumbia macho jinai kama hiyo kunadhoofisha itibari ya mfumo wa Umoja wa Mataifa.
Alfajiri ya tarehe 13 mwezi Juni mwaka huu utawala ghasibu wa Israel ulianzisha mashambulizi dhidi ya ardhi ya Iran kwa kulenga maeneo mbalimbali ya kijeshi na kuua shahidi idadi kadhaa ya makamanda wakuu wa kijeshi na wanasayansi wa nyuklia pamoja na raia wa kawaida.
342/
Your Comment