30 Juni 2025 - 13:39
Source: Parstoday
Maulamaa Wakuu wa Iran: Shambulio lolote dhidi ya Kiongozi Muadhamu ni jinai ya kivita

Maulamaa wakuu wa Kiislamu nchini Iran wamesema kuwa shambulio lolote au tishio dhidi ya Kiongozi Muadhamu na Marjai ni sawa na kutenda jinai ya kivita.

Ayatullah Mkuu Nasser Makarem Shirazi na Ayatollah Mkuu Hossein Nouri-Hamedani walitoa kauli hii katika fatwa zao za kidini siku ya Jumapili.

Ayatullah Makarim Shirazi amesema: "Kila mtu au Serikali yoyote itakayojaribu kuudhuru Umma wa Kiislamu na uongozi wake kwa kutishia au – Mwenyezi Mungu aepushie mbali – kumdhuru Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu au Marja wa Kishia, basi mtu au serikali hiyo itahesabiwa kuwa ni (adui) mpiganaji vita dhidi ya Uislamu (Muha'rib).

Ushirikiano au kuungwa mkono kwa namna yoyote ile watu au serikali hizo na Waislamu au nchi za Kiislamu ni haramu.

Ni wajibu kwa Waislamu kote duniani kuwafanya maadui hawa wajutie matamshi na vitendo vyao. Na ikiwa Waislamu watapata mashaka au hasara kutokana na kusimama dhidi yao, basi wao watakuwa na thawabu ya Mujahid (Mpiganaji katika Njia ya Mwenyezi Mungu), Insha'Allah."

Naye Ayatullah Noori-Hamedani amesema kuwa kumvunjia heshima Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, au Marja wa kishia ni sawa na kudhalilisha misingi ya Uislamu wenyewe.

Amefafanya kwa kusema: “Leo hii, Mheshimiwa Kiongozi Muadhamu anaongoza Umma wa Kiislamu kwa nguvu na ujasiri mkubwa. Hakuna shaka kuwa kumuunga mkono ni wajibu wa kila Muislamu, na kumdhoofisha ni haramu kabisa – hasa katika kipindi hiki ambacho maadui wa Uislamu, Qur’an na Ahlul-Bayt (amani iwe juu yao) wameungana.” 

Aidha amesema: “Shambulio lolote au tishio dhidi yake na Umarja wa Kishia, liwe linatoka kwa mtu binafsi au nchi, ni tendo la uadui wa wazi, na yeyote anayeshiriki katika jinai hiyo anachukuliwa kuwa na makosa kama wahusika wakuu."

Mnamo Juni 13, utawala wa Kizayuni wa Israel ulianzisha uvamizi wa kikatili dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ukiwaua makamanda wakuu wa kijeshi na wanasayansi wa nyuklia pamoja na raia wa kawaida, wakiwemo wanawake na watoto.

Aidha, utawala wa Kizayuni na Rais wa Marekani wametoa vitisho dhidi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei. Trump, kwa lugha yake ya matusi ya kawaida, siku ya Ijumaa alimshambulia Ayatullah Khamenei kwa maneno machafu, akidai kwamba aliuzuia utawala wa Israel na majeshi ya Marekani kumuua.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha