Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe wake ametoa rambirambi kufuatia kifo cha (A'lim) Mjuzi Mwanajihadi na Mtumishi, Hujjatul-Islam Sayyid Mohammad Shahcheraghi.
Andiko la ujumbe wa Kiongozi Muadhamu, Ayatollah Khamenei ni kama ifuatavyo:
Bismillahir-Rahmanir-Rahim
“Kifo cha A'lim Mwanajihadi na Mtumishi Marehemu, Hujjatul-Islam Bwana Haj Sayyid Mohammad Shahcheraghi, ninatoa rambirambi kwa watu wa heshima wa Mkoa wa Semnan, wapenzi na wafuasi wake, na hasa familia ya heshima ya Shahcheraghi na familia ya marehemu huyo.
Miaka mingi ya kuwa Imamu wa Ijumaa wa Semnan, ushirikiano wake na vipengele vya mapinduzi na vijana, pamoja na huduma zake nyingine kwa jamii, ni miongoni mwa sifa za kiongozi huyu mwema na inastahili fadhila za Kimungu. Rahma ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake.”*
Sayyid Ali Khamenei
14 / 12 / 2025
Your Comment