23 Desemba 2025 - 22:32
Je, , Beirut inaweza kuipokonya silaha Hezbollah ifikapo mwishoni mwa mwaka 2025?

Wachambuzi wanaonya kuwa ikiwa Beirut itaharakisha zoezi la kuipokonya silaha bila kupata mafanikio sambamba kutoka kwa Israel - kama vile kusitishwa kwa mashambulizi ya anga- hatua hiyo inaweza kuimarisha nafasi ya kisiasa na kijamii ya Hezbollah. Hii ni kwa sababu Hezbollah si kundi la kijeshi pekee, bali pia ni chama cha kisiasa chenye ushawishi mpana.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Uchambuzi wa gazeti la New York Times unaonyesha kuwa Lebanon ipo katika hatua nyeti na dhaifu; licha ya Hezbollah kurudi nyuma kijeshi na kupoteza sehemu ya uwezo wake baada ya vita, bado haijashindwa.


Ripoti hiyo inaeleza kuwa shinikizo la Marekani na Israel dhidi ya serikali ya Lebanon ili kuipokonya silaha Hezbollah kikamilifu kabla ya mwisho wa mwaka 2025 linaendelea, huku ikionya kwamba ongezeko dogo tu la mvutano kutoka Tel Aviv linaweza kufufua tena simulizi ya “upinzani”.


Kwa mujibu wa makala ya pamoja ya New York Times, baada ya kusitishwa kwa mapigano, Hezbollah imechukua hatua za kurudi nyuma kijeshi katika maeneo ya mipakani, na ghala lake la silaha limepata uharibifu. Hata hivyo, maafisa wa Magharibi wanasema kuwa kundi hilo linaendelea kujenga upya uwezo wake, jambo linaloongeza hofu ya kuzuka kwa duru mpya ya vita - hasa ikizingatiwa kuwa mashambulizi ya Israel dhidi ya malengo ndani ya Lebanon yanaendelea karibu kila siku.


Ufanisi wa mwisho wa zoezi la kuipokonya silaha Hezbollah unategemea mizani nyeti sana. Wachambuzi wanaonya kuwa ikiwa Beirut itaharakisha zoezi la kuipokonya silaha bila kupata mafanikio sambamba kutoka kwa Israel - kama vile kusitishwa kwa mashambulizi ya anga- hatua hiyo inaweza kuimarisha nafasi ya kisiasa na kijamii ya Hezbollah. Hii ni kwa sababu Hezbollah si kundi la kijeshi pekee, bali pia ni chama cha kisiasa chenye ushawishi mpana.


Kwa upande mwingine, gazeti la Al-Quds Al-Arabi linaandika kuwa juhudi za Hezbollah za kujijenga upya zinakabiliwa na changamoto kubwa.

Kuanguka kwa serikali ya Assad nchini Syria kumeikatiza njia muhimu ya usambazaji wa silaha na fedha. Aidha, ingawa Iran bado inatoa misaada ya kifedha isiyo rasmi, wachambuzi wanaamini kuwa msaada wa kikanda haukidhi tena kikamilifu gharama zinazoongezeka za kundi hilo.
Waziri Mkuu wa Israel kwa njia isiyo ya moja kwa moja anaonyesha kupendelea kuipokonya silaha Hezbollah kupitia serikali ya Lebanon badala ya vita kamili. Hata hivyo, mafundisho mapya ya kiusalama ya Israel yanasisitiza kuondoa vitisho vipya kabla havijarejesha kikamilifu nguvu zao. Tofauti hii ya mitazamo imeathiri mazungumzo ya kusitisha mapigano kati ya ujumbe wa Israel na Lebanon yanayosimamiwa na Marekani.


Serikali ya Lebanon, kwa lengo la kupata mabilioni ya dola za misaada ya kifedha kutoka Magharibi na nchi za Kiarabu, imejitolea kuonyesha maendeleo katika suala la kuipokonya silaha Hezbollah. Katika muktadha huu, Jeshi la Lebanon—kwa msaada na ushirikiano wa kiintelijensia usio wa kawaida kutoka kwa Israel - linaharibu maelfu ya silaha ili kujitokeza kama mhimili mkuu wa usalama wa taifa badala ya Hezbollah.


Wachambuzi wanaonya kuwa kuendelea kwa mashambulizi ya Israel kunaweza, bila kukusudia, kuimarisha simulizi ya “upinzani”.

Kwa mtazamo wa Beirut, kudhoofishwa kwa serikali ya sasa kupitia vita vipya kutakuwa kwa manufaa ya Hezbollah; kwa sababu hiyo, serikali ya sasa inaonekana kama “chaguo bora zaidi” kwa Israel ili kupunguza kwa ndani nguvu za kijeshi za Hezbollah.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha