19 Februari 2026 - 22:32
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi: Qur’an Tukufu iwe mzizi zaidi katika maisha yetu ya kila siku +Video

Kiongozi Muadhamu Sayyid Ali Khamenei amewapongeza Wasomaji wa Qur’an katika Kikao maalumu cha Usomaji wa Qur’an Tukufu, akisisitiza kwamba Qur’an iwe sehemu ya kila siku ya maisha ya Waislamu. Alibainisha kuwa usomaji wa Qur’an husaidia uimarishaji wa Nafsi ya mja, na kuendeleza uhusiano wa mtu na Mwenyezi Mungu, na kuwa msingi wa thawabu na baraka zinazoongezeka siku hadi siku.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Baada ya Programu ya kusoma Qur’an, ambapo waumini wakiongozwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ilifuatia neno la shukrani kutoka Kwa Kiongozi Muadhamu kwa wasomaji wa Qur’an ambapo aliwatakia  kila mema, Baraka na neema tele katika Usomaji wa Qur'an Tukufu, na alisema:

"Ilifanyika vizuri sana, tulifaidika sana. Insha’Allah kila wakati wawe na Qur’ani karibu na mioyo yao, na kwamba kila siku msitu mdogo wa Qur’ani ukuwe zaidi na zaidi."

Kiongozi Mkuu aliendelea kusisitiza umuhimu wa Qur’ani katika maisha ya kila siku ya Waislamu, akihimiza kwamba usomaji na tafsiri yake iwe sehemu ya maisha ya kiroho, ikisaidia kuimarisha uhusiano na Mwenyezi Mungu na kuendeleza thawabu za kiroho.

Ramadhan, mwezi wa Qur’ani Tukufu, unatoa fursa ya pekee kwa Waislamu kusoma, kuelewa, na kutekeleza mafundisho yake, huku kila sala, doa, na usomaji ukipandisha thawabu na kumkaribia Mtukufu.

Your Comment

You are replying to: .
captcha