Jaji Richard Leon alisema kuwa tabia hiyo inaingilia taarifa za faragha za watu na kuwa haistahili na pia wamarekani hawaishi kwa amani kwani simu zao zote zinachunguzwa.siri hii ya Marekani kuchunguza taarifa binafsi na taarifa za siri za viongozi wa nchi nyingine ilifichuliwa na jasusi wa Marekani aliyetoroka Edward Snowdon. Jaji Leon alitoa agizo la muda la kuzuia shirika hilo kuendeleza upelelezi huo ulio kunyume na sheria.
16 Desemba 2013 - 20:30
News ID: 489294

Jaji wa mahakama nchini Marekani amesema kuwa tabia ya shirika la ujasusi la Marekani kukusanya taarifa kwenye simu za watu binafsi ni kinyume na katiba ya nchi hiyo.