Jeshi la Iraq limefanikiwa kukomboa kambi mbili za kijeshi kutoka katika mikono ya magaidi wa Daesh.
Mafanikio haya yamekuja baada ya mapambano makali yaliyofanywa najeshi Iraq likishirikiana na wananchi waliojitolea kupambana na magaidi, katika mji wa Anbal Magharibi mwa nchi hiyo.
Kikundi cha magaidi wa Daesh kiliteka kambi ya jeshi la Iraq katika mji wa Anbal na kuwateka wanajeshi mia mbili wa Iraq.
pia waliteka kambi ya jeshi nyingine iliyipo kaskazin mwa mji wa Falujah katika kitongoji cha Saqlawiyah, ambapo magaidi hawa waliua wanajeshi wa Iraq 700.
viongozi wa Iraq na Syria wamekuwa wakizilaumu serikali za Saudia Arabia, Uturuki,Qatar na baadhi ya nchi za Ghuba ya Uajemi kwa kuwaunga mkono magaidi, pia serikali za Iraq na Syria zimeishukuru serikali ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran kwa kuzisaidia katika kupambana na magaidi hao.
Ni muhimu kuashiria kamba, bila jeshi la Iran, serikali za Syria na Iraq zingekuwa zimekwisha angushwa, jeshi la Iran limekuwa likiisaidia Syria kupambana na magaidi tangu mwaka 2011.
26 Septemba 2014 - 08:54
News ID: 640327

Jeshi la Iraq limefanikiwa kukomboa kambi mbili za kijeshi kutoka katika mikono ya magaidi wa Daesh.