Magaidi wa kikundi cha Nusra ambacho ni tawi la Al-qaida kinachofanya mapambano dhidi ya serikali ya Bashal Asad wa kimetoa onyo kali kuhusiana na mashambulizi ya anga ya Marekani huko Syria.
Kiongozi wa kundi hilo la kigaidi Abu Mohammad al-Golani alinukuliwa akisema"WamarekaniJe mmesahau tulivyokupeni hasara na kuua askari wenu Iraq,Afghanistan na Somalia? Je mmesahau tukio la kutisha la Septemba 11? Je mmesahau meli yenu ya kivita iloshambuliwa Yemen? na Je mmesahau matukio yote tunayoyafanya kwenye miji yenu?"
Aliendelea kwa kusema" nawasikitikia Marekani na washirika wake kama watakuwa wamesahau hasara walizopata na wanazoendelea kupata katika kuendesha vita hivi"
Abu Mohammad al-Golani aliendelea kusema kuwa: hapana shaka kwamba wao ndio watakao shinda katika vita hivi,
Pia aliwaomba wanajeshi wa Lebanon walio katika dhehebu la Sunni, waachane na jeshi lao, na kujiunga na kikundi chao.
Ni muhimu kuashiria kwamba tangu september 22, Marekani na washirika wake wameanza mashambulizi ya anga dhidi ya makundi ya kigaidi ya Syria na Iraq, makundi mbali mbali ya kikagaidi yalianza mashambulizi yake nchini Syria tangu mwaka 2011, kwa lengo la kuangusha serikali ya Bashar asad lakini yameshindwa kufikia lengo lao kutokana na himaya nzito anayoipata Bashar asad kutoka kwa jeshi la Iran na kundi la Hizbollah.
29 Septemba 2014 - 07:46
News ID: 641007

Magaidi wa kikundi cha Nusra ambacho ni tawi la Al-qaida kinachofanya mapambano dhidi ya serikali ya Bashal Asad wa kimetoa onyo kali kuhusiana na mashambulizi ya anga ya Marekani huko Syria.