-
Brazil yamrejesha nyumbani balozi wake wa Israel kulalamikia jinai za Gaza
Brazil imemrejesha nyumbani balozi wake wa Israel kulalamikia mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza, ambayo yamepelekea Wapalestina zaidi ya 36,100 kuuawa shahidi tangu Oktoba, 2023.
-
Maandamano ya kuunga mkono Palestina yaendelea Ulaya licha ya ukandamizaji wa polisi
Kwa siku ya tatu mfululizo, Ufaransa inashuhudia maandamano makubwa ya kuunga mkono Palestina na kupinga mauaji ya kimbari yanayoendelezwa na utawala haramu wa Israel huko Gaza na pia mauaji ya hivi karibuni kabisa yaliyotekelezwa na utawal wa Israel huko Rafah.
-
Trump aapa "kutimua wanafunzi" na kukandamiza wanaounga mkono Palestina akichagualiwa tena kuwa rais
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameapa kuwa atakandamiza maandamano ya watetezi na waungaji mkono wa Palestina yanayoendelea kufanywa katika vyuo vikuu vya nchi hiyo na kusisitiza kuwa "atawafukuza" wanafunzi wanaohudhuria maandamano hayo, ikiwa atachaguliwa kurudi tena madarakani.
-
Licha ya mauaji ya Rafah, US yasema Israel bado haijavuka 'mstari mwekundu' wa Biden
Msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa la Marekani John Kirby amedai kuwa Israel haijakiuka "mstari mwekundu" wa Rais Joe Biden wa kuifanya Washington isitishe katika siku za usoni kuipatia Tel Aviv silaha za mashambulizi kwa sababu inavyohisi Marekani Israel haitaanzisha operesheni ya ardhini ya kuuvamia kikamilifu mji wa Rafah wa kusini mwa Ukanda wa Ghaza.
-
Donald Trump akiri juu ya udhaifu wa utawala wa Kizayuni
Donald Trump, Rais wa zamani wa Marekani amesema katika mkusanyiko wa Wayahudi wa Marekani kwamba utawala wa Israel umepoteza uwezo wake.
-
WHO: Dunia imetimiza nusu tu ya lengo la kimataifa la huduma muhimu za afya ifikapo 2025
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani amesema licha ya hatua kubwa ya upashaji habari, ni watu milioni 585 tu ambao watafikiwa na huduma muhimu za afya ifikapo mwaka 2025.
-
Umoja wa Mataifa: Changamoto za ulimwengu zinaongezeka huku afya ikizorota
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, changamoto zinazoukabili ulimwengu hivi sasa zimekuwa zikiongezeka kila sikuu huku hali ya afya ikizorota.
-
Takwa la Bunge la Kiarabu la kusimamishwa mara moja mauaji ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza
Katika kikao kilichofanyika katika makao makuu ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu mjini Cairo, Spika wa Bunge la Kiarabu ametaka kusitishwa mara moja jinai na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Radiamali ya jamii ya kimataifa kwa ushirikiano wa utawala ghasibu wa Israel na Marekani
Wawakilishi wa Misri na Russia katika Umoja wa Mataifa wamesisitiza juu ya ulazima wa jamii ya kimataifa kukabiliana na jinai za utawala ghasibu wa Israel.
-
Wanasheria wa The Hague waunga mkono ombi la kukamatwa viongozii wa Israel
Wataalamu na mawakili wa kujitegemea mjini The Hague wameunga mkono uamuzi wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ya kuomba hati ya kukamatwa maafisa wa utawala ghasibu wa Israel.
-
Afisa Myahudi katika serikali ya Biden ajiuzulu kulalamikia mauaji ya kimbari ya Ghaza
Lily Greenberg Call, msaidizi maalumu wa mkuu wa wafanyakazi katika Idara ya Mambo ya Ndani ya serikali ya Marekani amekuwa mteuliwa wa kwanza wa kisiasa wa Kiyahudi kujiuzulu hadharani akipinga uungaji mkono wa Washington kwa mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika katika Ukanda wa Ghaza uliowekewa mzingiro.
-
Maandamano ya kuunga mkono Palestina na Ghaza yaendelea katika miji mbalimbali duniani
Watu wa miji tofauti katika nchi mbalimbali duniani, kwa mara nyingine wamemiminika mabarabarani wakiandamana kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina hususan wa Ukanda wa Ghaza na kulaani jinai za mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala dhalimu wa Kizayuni wa Israel katika eneo hilo.
-
Madai ya Marekani ya kusimamisha kuupelekea silaha utawala wa Kizayuni wa Israel
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alidai siku ya Jumatano mbele ya Baraza la Seneti la nchi hiyo kwamba kuupelekea silaha utawala wa Kizayuni wa Israel kumesimamishwa kwa sababu ya utawala huo kutekeleza operesheni ya kuivamia kijeshi Rafah, lakini pamoja na hayo bado hawajachukua uamuzi rasmi kuhusu hatima ya shehena hiyo ya silaha.
-
Seneta wa Marekani: Wanafunzi wanaopinga vita vya Ghaza wamesimama upande sahihi wa historia
Bernie Sanders, Seneta wa kujitegemea anayewakilisha jimbo la Vermont nchini Marekani amewasifu wanafunzi wa vyuo vikuu vya nchi hiyo wanaopinga vita katika Ukanda wa Ghaza na kusema, wanafunzi hao wamesimama upande sahihi wa historia.
-
Ufaransa yamzuia daktari Muingereza aliyekuwa Gaza kuingia nchini humo kutoa ushahidi
Daktari mpasuaji mwenye uraia pacha wa Uingereza na Palestina, Ghassan Abu Sittah ambaye ni shahidi wa uhalifu wa kivita wa Israel katika Ukanda wa Gaza, amezuiwa kuingia Ufaransa, ambako alipangwa kuhutubia Baraza la Seneti kuhusu hali ya Gaza.
-
Sisitizo la Iran kuhusu Palestina kupewa uanachama kamili katika Umoja wa Mataifa
Amir Saeid Iravani, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesisitiza umuhimu wa Palestina kuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa.
-
Wanajeshi wa Russia waingia kambi ya wanajeshi wa Marekani nchini Niger
Wanajeshi wa Russia wameingia katika kambi ya Jeshi la Anga la Niger ambayo pia ina wanajeshi wa Marekani baada ya serikali ya Niger kuamuru vikosi vya jeshi la Marekani kuondoka nchini humo.
-
Trump: Nikichaguliwa kuwa Rais nitarejesha marufuku ya Waislamu kuingia Marekani
Donald Trump mgombea anayetarajiwa kuteuliwa na chama cha Republican kuwania kkiti cha urais nchini Marekani amesema kuwa, akichaguliwa atarejesha tena marufuku ya kusafiri kwa baadhi ya nchi zenye Waislamu wengi katika siku ya kwanza ya utawala wake mpya.
-
Kuongezeka ukatili dhidi ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Marekani wanaounga mkono Palestina
Huku maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Marekani yakiendelea kufanyika kwa lengo la kupinga jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza na vilevile kwa ajili ya kuwaunga mkono Wapalestina, polisi wa nchi hiyo wameongeza hatua zao za ukandamizaji dhidi ya wanafunzi hao.
-
Kukatwa kikamilifu uhusiano wa Colombia na utawala wa Kizayuni; kuendelea kutengwa Tel Aviv kimataifa
Rais Gustavo Petro wa Colombia alisema siku ya Jumatano tarehe Mosi Mei katika hotuba yake kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kuwa kuanzia Alhamisi amekata kikamilifu uhusiano wa nchi hiyo na utawala wa Kizayuni kwa sababu ya jinai na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo huko Ukanda wa Gaza.
-
Colombia yaamua kuvunja uhusiano na Israel kwa sababu ya mauaji ya kimbari ya Ghaza
Colombia imeamua kuvunja uhusiano wake wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na vita vya kinyama na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala huo haramu dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.
-
Wanachuo wanaoitetea Palestina Marekani watiwa nguvuni Texas, wasimamishwa masomo Columbia
Polisi nchini Marekani wamekabiliana na wanafunzi wa chuo kikuu katika mji wa Austin jimboni Texas, na kuwakamata makumi ya watu baada ya kubomoa mahema yaliyowekwa kupinga na kulalamikia vita vya kinyama na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ghaza.
-
Wasiwasi wa Russia kuhusu kusambaa zaidi ugaidi kutokea Afghanistan
Waziri wa Ulinzi wa Russia ametangaza kuwa tishio kuu kwa Asia ya Kati ni kutoka kwa makundi ya kigaidi yenye misimamo mikali yenye makao makuu nchini Afghanistan.
-
Mgombea wa uchaguzi wa rais Marekani atiwa nguvuni katika maandamano ya watetezi wa Palestina
Polisi nchini Marekani imemtia nguvuni mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka huu nchini humo ambaye alikuwa katika maandamano ya kuiunga mkono Palestina yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Washington.
-
Wanafunzi wanaunga mkono Palestina waendelea kukamatwa Marekani
Katika siku za hivi karibuni, polisi nchini Marekani wamewatia mbaroni wanafunzi wa vyuo vikuu wasiopungua 900 wanaoiunga mkono Palestina na wanaopinga mauaji ya kimbari ya utawala ghasibu na haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza
-
Raisi: Mkono wa chuma hauwezi kuzima harakati ya wanachuo Magharibi ya kuunga mkono Palestina
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, harakati ya wanafunzi, maprofesa na wasomi wa nchi za Magharibi za kuwaunga mkono wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina ni tukio kubwa lenye muelekeo mipana ambalo haliwezi kuzimwa kwa ukandamizaji, vipigo, kamatakamata na vitendo vya utumiaji mabavu.
-
UN yaunga mkono maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu Marekani ya kuwatetea watu wa Gaza
Stephen Dujaric Msemaji wa Umoja wa Mataifa jana Ijumaa alisema katika radiamali yake kwa maandamano yanayoendelea kufanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu huko Marekani katika kuwaunga mkono watu wa Gaza na kupinga mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa eneo hilo kwamba: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni mfuasi na mungaji mkono mkubwa wa uhuru wa kujieleza, ikiwa ni pamoja na huko Marekani; na anaunga mkono haki ya wananchi ya kufanya maandamano kwa amani.
-
Marekani ya 'kidemokrasia' yakandamiza wanachuo wanaopinga unyama wa Israel, 500 wakamatwa
Polisi wa Marekani wamewakamata zaidi ya waandamanaji 500 wakati wa msako mkali dhidi ya waandamanaji wanaounga mkono Palestina kwenye kampasi za vyuo vikuu kote nchini humo.
-
Marekani yashadidisha ukandamizaji dhidi ya wapinzani wa utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wa Palestina
Marekani ndiyo muungaji mkono mkubwa zaidi wa utawala wa Kizayuni wa Israel ambapo serikali ya Biden imetoa msaada mkubwa zaidi wa kijeshi na silaha kwa Tel Aviv wakati wa vita vya Gaza, ambavyo vimeingia katika mwezi wake wa saba.
-
Mtaalamu wa UN ataka Israel iwekewe vikwazo vya silaha, mafuta
Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ardhi ya Palestina Inayokaliwa kwa Mabavu Francesca Albanese ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuweka vikwazo vya mafuta na silaha dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel unaoendeleza mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.