22 Mei 2024 - 18:58
Wanasheria wa The Hague waunga mkono ombi la kukamatwa viongozii wa Israel

Wataalamu na mawakili wa kujitegemea mjini The Hague wameunga mkono uamuzi wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ya kuomba hati ya kukamatwa maafisa wa utawala ghasibu wa Israel.

 ujumbe wa wataalamu na mawakili wa kujitegemea kutoka mjini The Hague umetangaza katika taarifa  yake kwamba, ombi la Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai la kutaka kuwakamata maafisa wa utawala ghasibu wa Kizayuni ni la haki na sahihi.

Jopo la wataalamu na wanasheria huru wa mjini The Hague wametangaza kuwa, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai imechukua hatua ya kihistoria ya kuhakikisha haki inatendeka kwa wahanga kwa kutoa ombi la kutaka kukamatwa kwa maafisa wa utawala ghasibu wa Kizayuni wanaoendeleza mauaji huko ukanda wa Gaza Palestina.Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel, alikejeli ombi la Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai la kutaka kumkamata na kudai kuwa, licha ya uamuzi huo atazunguka dunia nzima akifanya safari zake kama kawaida bila woga. Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamini Netanyahu alidai kuwa jaribio la mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICJ) la kutoa hati ya kukamatwa maafisa wa utawala huo wa Kizayuni ni la kipuuzi na litaisababishia fedheha kubwa mahakama hiyo. Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ilitangaza Jumatatu iliyopita mwezi Mei tarehe 20, 2024 kwamba imetoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Waziri wake wa Vita Yoav Gallant, Waziri wa Vita wa utawala wa kibaguzi wa Israel kwa tuhuma za uhalifu wa kivita wanaoutenda huko ukanda wa Gaza. Uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai wa kutoa hati ya kukamatwa kwa baadhi ya maafisa wa utawala ghasibu wa Kizayuni kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Waziri wake wa Vita Yoav Gallant, umefuatiiwa na radiamali mbalimbali.

342/