Ujerumani imesikitishwa sana na kile imekitaja kuwa ni "ukatili mkubwa" shambulizi lililofanywa na Taliban ambalo limewauwa karibu watu 132, wengi wao watoto, katika shule moja inayosimamiwa na jeshi ya mji wa kaskazini mashariki mwa Pakistan, Peshawar.

16 Desemba 2014 - 18:24

 Waziri wa Mambo ya Kigeni Frank-Walter Steinmeier amesema katika taarifa kuwa kitendo hicho cha kuwateka nyara na kuwauwa watoto ni unyama usiowahi kushuhudiwa Pakistan ambayo kwa miaka mingi imekumbwa na ugaidi na machafuko. Mjini Paris, Rais wa Ufarasna Francois Hollande amesema Ufaransa "inaunga mkono serikali ya Pakistan katika vita dhidi ya ugaidi" na akaeleza mshikamano wake na wahanga wa shambulizi hilo. Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amelaani shambulizi hilo la "woga" akisema ni kitendo kibaya na ukatili usioweza kuzungumzwa. Walioshuhudia walieleza namna watu waliokuwa na silaha walivyoingia katika darasa moja hadi jingine, wakiwapiga risasi wanafunzi, baada ya mlipuko mkubwa kuitikisa shule hiyo ya umma inayosimamiwa na jeshi. Kundi la Taliban limedai kuhusika likisema ni hatua ya kulipiza kisasi operesheni kubwa ya kijeshi iliyofanywa katika eneo hilo, likisema wanamgambo walipewa maagizo ya kuwauwa kwa risasi watoto wenye umri mkubwa.

Tags