Main Title

source : Parstoday
Jumanne

22 Agosti 2023

18:22:31
1388677

Korea Kaskazini: Lengo la mkutano wa Camp David ni uchochezi wa kuanzisha vita vya nyuklia

Korea Kaskazini imesema, lengo la mkutano wa viongozi wa Marekani, Korea Kusini na Japan uliofanyika Camp David Ijumaa iliyopita ni uchochezi wa kuanzisha vita vya nyuklia.

Siku ya Jumatatu, Korea Kusini na Marekani zilianza mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyopewa jina la Ngao ya Uhuru ya Ulchi (Ulchi Freedom Shield) yaliyoratibiwa kwa lengo la kuimarisha hatua za pamoja za kilichotajwa kuwa ni kujibu mapigo kwa vitisho vya nyuklia na makombora vya Korea Kaskazini. Kwa muda mrefu Pyongyang imekuwa  ikilaani manuva hayo ambayo imeyaita mazoezi ya kujiandaa kwa vita.   Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA; Korea Kaskazini jana Jumanne ilitoa taarifa ya kulaani mazoezi ya kila mwaka ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini na kusema kwamba mkutano wa viongozi wa Marekani, Korea Kusini na Japan uliofanyika Camp David unaongeza uwezekano wa kutokea vita vya nyuklia.  

Korea Kaskazini imesisitiza kuwa, kutokana na hali iliyopo kuna ulazima kwa jeshi la nchi hiyo kubuni hatua za kuchukua na kujipanga kwa ajili ya mashambulizi madhubuti ya kivita.   Jana asubuhi,  Pyongyang ilifanikiwa kufanyia majaribio makombora yake ya kimkakati ya cruise kutokea kwenye manowari. Jaribio hilo lilifanyika mbele ya kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un.   Korea Kaskazini imeshatangaza mara kadhaa kuwa itaendelea kuongeza nguvu na uwezo wake wa kijeshi hadi pale Marekani na washirika wake wa ukanda wa Peninsula ya Korea watakapoacha vitendo vya uharibifu na vya uzushaji mivutano dhidi ya nchi hiyo.../

342/